Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba ya Uturuki kujifua Uwanja wa Uhuru leo

10322 Pic+simba TanzaniaWeb

Mon, 6 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Simba wametua alfajili ya leo wakitokea Uturuki na jioni watafanya mazoezi yao ya kwanza kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mazoezi hayo yatatoa nafasi kwa mashabiki wao kuona wachezaji wao kwa mara ya kwanza wakijifua na kuonyesha mavitu na ufundi waliopata Uturuki

Akizungumza baada ya kuwasili nchini Kocha wa Simba, Mbeligiji Patrick Aussems alisema amefurahishwa na viwango vya wachezaji wake ambao amekutana nao kwani hakutegemea kukutana na wachezaji wa aina hiyo.

Alisema mbali ya kuwa na uwezo wanajituma na wanakiu ya kuona wanapata mafanikio kitimu na wao binafsi.

"Maandazi ambayo tumeyafanya katika kambi yetu hii ni mazuri na kwa yale ambayo tulikuwa tunahitajika kama benchi la ufundi tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

"Nadhani ni wakati muafaka wa kuonyesha kile ambacho tumekipata katika maandalizi yetu haya haswa katika kila mechi kwani kila kitu tulikuwa tukapata kwa wakati.

"Niwapongeze pia viongozi kwa kuona umuhimu wa timu kuweka kambi nje ya nchi kwani ni ishara tosha wanakiu ya kuona timu inafanya vizuri zaidi ya msimu uliopita," alisema Mbelgiji huyo.

"Mashabiki wajitokeze kwa wingi katika mechi na Asante Kotoko kwani ni kipimo sahihi kwetu kwa maandalizi ambayo tumeyafanya," alisema Aussems.

Chanzo: mwananchi.co.tz