Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba watoa angalizo kwa watoa ahadi

Simba Piic Data Simba watoa angalizo kwa watoa ahadi

Sat, 2 Oct 2021 Chanzo: eatv.tv

Mshauri wa Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Crecentius Magori amewataka Viongozi wa wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa wasitoea hela na waache timu zicheze mpira kwakuwa anaamini timu yenye uwezo itapata matokeo.

Kauli hiyo imetolewa baada ya mchezo wa jana kushuhudiwa beki wa Simba, Kennedy Juma  kufanyiwa rafu na mchezaji wa Dodoma Jiji na kushindwa kumaliza mchezo wa Ligi Kuu uliomalizika kwa wekundu wa msimbazi kushinda bao 1-0.

''Tunasikia watu wanaagiza mahela, naskia Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa, ndio yanasabisha watu wanakamia mechi hata kama hawana uwezo lakini wanaharibu mpira''Crecentius Magori.

Katika mchezo wa jana wachezaji watatu wa Simba, Ousmane Sakho, Thaddeo Lwanga na Kennedy Juma hawakumaliza mchezo kutokana na majeraha.

Simba inakamata usukani wa Ligi Kuu ikiwa na alama 4 baada ya kucheza michezo miwili iliyocheza ikiwa imepata ushindi mmoja na sare moja.

 

Chanzo: eatv.tv