Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba watambia kikosi chao

D1e8ad471bc9f3c65db115aefba3029d Simba watambia kikosi chao

Sat, 29 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KLABU ya Simba imesema ubora wa kikosi chake ni moja ya sababu inayowaweka kwenye mazingira mazuri ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Namungo FC unaotarajiwa kupigwa kesho jioni kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

Mchezo huo utafanyika kwa kuzikutanisha Simba, ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Namungo iliyofanya vyema kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam( FA) ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu kwa mwaka 2020/2021 utakaoshiorikisha klabu 18.

Akizungumza kutoka Arusha kocha msaidizi wa Simba, Sulemani Matola alisema mchezo huo utakuwa mgumu kwakuwa kila upande una matamanio ya ushindi ili kuchukua ngao hiyo.

Alisema anaamini bado wana kikosi bora kabisa ikilinganishwa na wapinzani wao, ambaoni wageni katika soka la Tanzania.

“Licha ya usajili tuliofanya kwa kuongeza wachezaji wapya, bado kikosi chetu ni bora kuliko wapinzani wetu, mchezo utakuwa na ushindani lakini naamini tuna nafasi kubwa ya kupata ushindi ili kujipanga na mchezo wetu wa kwanza wa ligi dhidi ya Ihefu FC,” alisema Matola.

Alisema ushindani wa mchezo huo unatokana na timu hizo kujuana kwani kwa msimu uliopita walikutana mara mbili kwenye mechi za ligi, ambapo Simba walishinda mechi moja na nyingine walitoka suluhu na walipokutana kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (FA) wekundu hao walifanikiwa kubeba ubingwa kwa kushinda mabao 2-1.

Alisema kikubwa bado wanawaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono kwa kuwashangilia wachezaji kwa wakati wote watakapokuwa wanaipigania timu kupata ushindi utakaowafanya kushinda na kujitengenezea mazingira ya kuanza kufanya vizuri kwenye michezo yao ya ligi.

Chanzo: habarileo.co.tz