Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wanashinda hadi mchangani

63837 Pic+gwambina

Sat, 22 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

MABINGWA wa Ligi Kuu Bara, Simba wameshinda mechi ya kirafiki dhidi ya Gwambina FC kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao moja ndani ya dakika 90.

Mchezo huo ambao ulikuwa maalumu pia kuitambulisha timu hiyo ya gwambina inayojiandaa kushiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao pamoja na kuzindua uwanja wao wa Gwambinaulioko wilayani hapa.

Gwambina FC ndio walioanza kutikisa nyavu za wapinzani wao dakika ya 50 kupitia Anwar Jabil baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Simba ambapo mlinda mlango, Deogretius Munishi 'Dida' alishindwa kuokoa hatari hiyo.

Hata hivyo dakika ya 85, Simba ilijibu mapigo kutia kiungo wake Said Ndemla alisawazisha bao hilo kwa mpira wa faulo baada ya kufanyiwa madhambi na Ibrahim Ngecha dakika ya 84.

Baada ya dakika 90 kumalizika na kutopatikana mshindi, mwamuzi Frednand Chacha aliamuru kupigwa penalti ambao upande wa Simba waliopiga penalti ni Ndemla, Yusuph Mlipili, Hassan Dilunga na Ben Jacob.

Upande wa Gwambina FC penalti zao zilipigwa na Yusuph Mfaume, Kalaga Mbino ambao walifunga huku Bruno John na Meshack Abraham wakikosa penalti hizo.

Chanzo: mwananchi.co.tz