Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wamejipanga kwa krosi zote

Krosi Pic Data Simba wamejipanga kwa krosi zote

Sat, 22 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KATIKA mechi ya kwanza Simba walifungwa mabao 4-0 dhidi ya Kaizer, lakini matatu kati ya hayo walifungwa kwa vichwa ambayo yalitokana na krosi mbili pamoja na kona moja.

Kwenye tizi la wiki hii pale Tegeta, Mwanaspoti ilishuhudia Didier Gomes akiwakomalia mabeki wake, Pascal Wawa, Joash Onyango, Kennedy Juma, Ibrahim Ame, Gadiel Michael, David Kameta, Kapombe na Tshabalala kuruka na kuokoa mipira hiyo.

Muda mwingi krosi na kona ambazo zilipigwa mabeki hao kila mmoja kwa nafasi yake aliokoa mipira hiyo na huenda katika mechi ya marudiano wakabadilika na mashabiki wakafurahi.

“Tumejaribu kufanyia tena kazi hili kwani ni moja ya makosa tuliyofanya katika mechi iliyoyapita na nina imani awamu hii halitatokea tena bao kama ambavyo tulifungwa katika mechi ya awali,” alisema Gomes.

TIZI LA MAKIPA

Kocha wa makipa Milton Nienov naye alikuwa amewakomalia makipa Aishi Manula, Benno Kakolanya na Ally Salim ambao walipewa mazoezi ya kucheza krosi, mashuti ya mbali, kona na mengine magumu.

“Tunafanyia kazi makosa ya kila mechi ambayo yatajitokeza huku nikiendelea kuwapa mbinu na vitu vipya katika kutimiza majukumu yao kwa ubora,” alisema Milton akisisitiza kwamba anaamini vijana wameiva na leo kutaonekana mabadiliko makubwa.

CHAMA NA BWALYA

Chama na Bwalya wao walipewa kazi mbili mazoezini kuhakikisha wanatengeneza nafasi za kufunga, kisha na wao kupiga mashuti nje ya boksi pamoja na kufunga aina nyingine ya mabao kulingana na nafasi ilivyotokea.

Gomes alisema wamefanya zooezi hilo ili kuhakikisha wanatengeneza nafasi nyingi za kufunga na kadri ambavyo wanazipata lengo likiwa kuivusha Simba.

“Tunahitaji ushindi mkubwa na ili tufanikiwe katika hilo ni lazima tutengeneze nafasi za kutosha za kufunga mabao tofauti na mechi ya kwanza na ziwafikie wachezaji sahihi wa kuzitumia. Nina imani itakuwa hivyo,” alisema Gomes.

IMEANDIKWA NA THOBIAS SEBASTIAN, CLEZENCIA TRYPHONE NA OLIVER ALBERT

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz