Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba walamba Sh 150 milioni

69535 Simba+coco+picha

Sat, 3 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KLABU ya Simba, leo Ijumaa ilitembelea ofisi za wadhamini wao wakuu Sportpesa zilizopo Coco beach hapa Dar es Salaam.

Mara baada ya kufika walitembezwa katika vyumba na maeneo mbalimbali ya ofisi hizo kuoneshwa kazi ambavyo zinafanyika.

Baada ya hapo Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji kutoka SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba alisema, aliwakabidhi kombe la Ligi Kuu Bara na nahodha msaidizi wa klabu hiyo, Mohammed Hussein 'Tshabalala'.

Baada ya kukabiziwa kombe, Tarimba aliwakabidhi Simba hundi ya Sh 50 milioni.

Tarimba alisema watawapa Simba zawadi ya Sh 150, milioniĀ  kutokana na kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita na kufika hatua ya robo faibali Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Tutawapa Sh 50, milioni kwa ajili ya kufika hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika, Sh 100, milioni kwa ajili ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara zawadi hizi ni nje ya mikataba yao," alisema Tarimba.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori alisema mafanikio hayo ni kutokana na nguvu ambayo wanaipata kutoka kwa wadhamini wao SportPesa.

"Tunawahidi wadhamini wetu kwa zawadi hii ya pesa ambayo watatupatia imetuongezea kufanya vizuri msimu uliopita na tutafanya vizuri msimu ujao," alisema Magori.

Chanzo: mwananchi.co.tz