Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba waitaka Yanga fainali

Shabiki Pic Data Simba waitaka Yanga fainali

Sat, 26 Jun 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MASHABIKI wa Simba waliopo nje ya uwanja wa Majimaji mjini Songea wakisubiri kuingia uwanjani kushukudia mechi ya nusu fainali ya Kombe la Azam (ASFC), kati ya chama lao na Azam wametema nyongo kuwa wanaitaka Yanga fainali.

Ikiwa tayari Yanga imefuzu kucheza fainali ya kombe hilo jana baada a kuichapa bao 1-0 Biashara United, mashabiki hao wa Simba wamesema wanahitaji kushinda mechi ya leo dhidi ya Azam ili kukutana na watani wao wa jadi Yanga kwenye fainali.

“Inyeshe mvua, liwake jua, lazima tushinde mechi ya leo ili tukakutane na Yanga kwenye fainali tuwashikishe adabu.

Wanampango wa kutukwepa Julai 3, sasa tunataka tukiwakosa hapo tuwapate huku maana hawawezi kutukwepa kote,” amesema Kharifa Juma kwa niaba ya mashabiki wenzake waliokuwa wakipiga ngoma nje ya uwanja.

Pia mwanamama aliyejitamvulisha kwa jina la Mama wa Msimbazi, aligongengelea msumari tambo hizo kwa kwa kusema.

“Tunaenda kumtoa Azam kisha tumfuate Yanga fainali, tunataka kuthibitisha kuwa sisi ndio magwiji na mabingwa wa makombe yote Tanzania,” amesema.

Saa9:30 jioni ndio muda ambao mechi ya Azam na Simba itaanza kwenye dimba la majimaji songea kutafuta mshindi atakaye ungana na Yanga kucheza fainali ya kombe la Azam.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz