Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wagoma kisa GSM

Gsmpic Data Simba wagoma kisa GSM

Fri, 10 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

UONGOZI wa klabu ya Simba kupitia kwa kitengo cha habari kinachoongozwa na Ally Shantri ‘Chico’ wamegoma kufanya kikao cha kocha na waandishi wa habari kisa bango lenye nembo ya GSM.

Mkutano wa makocha kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Simba na Yanga ulikuwa unafanyika leo katika makao makuu ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF).

Kocha wa Yanga, Nassredine Nabi ndiye aliyeanza kuzungumza na alipomaliza msemaji wa TFF, Clifford Ndimbo aliwataka Simba waingie lakini waligoma.

Chico alisikika akisema ”toeni bango kwanza”.

Baada ya Simba kugoma kuingia Ndimbo aliwaruhusu wadhamini wakuu wa Ligi, NBC kuingia na kuzungumziq mchezo huo.

Ikumbukwe toka wiki iliyopita Simba waliandika barua ya kuomba ufafanuzi juu ya udhamini wa TFF na GSM walioingia na kutaka nembo ya kampuni hiyo kuwa sehemu ya jezi.

Advertisement Mwanaspoti ambalo lilishuhudia magari mawili ya Simba yakiingia Harrier (Rabi Hume) na Mercedes Benz (Barbara Gonzalez, Chico na Pablo Franco) baada ya kugoma kuingia Rabi na Chico walitoka kisha wakaondoka kwa pamoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live