Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba waahidi kishindo usajili

62580 Pic+usajili

Thu, 13 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Klabu ya Simba imetamba kufanya usajili wa kishindo katika kipindi hiki kwa kuleta nyota watakaoimarisha kikosi chao msimu ujao.

Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba, Crescentius Magori alisema kuwa klabu hiyo haina presha katika ufanyaji usajili na wamekamilisha mchakato huo kwa asilimia kubwa.

"Zoezi la usajili linaendelea na wapo wachezaji ambao tutawaacha ama kuwatoa kwa mkopo, lakini siwezi kuwatangaza hapa lakini pia kama mnavyoona kila siku tunaongezea mchezaji mkataba.

Wapo wachezaji wa ndani ambao tumeshakamilisha na baada ya hapo tutaanza kuwatangaza wachezaji wa kimataifa. Niwahakikishie kuwa safari hii wachezaji wa kigeni tutakaowasajili ni wale ambao wana uwezo mkubwa kuliko ambao tutawaacha. Ni wachezaji ambao hata mkienda kuwafuatilia, wasifu wao ni mkubwa," alisema Magori

Chanzo: mwananchi.co.tz