Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba sc Yatamba Kuishangaza Afrika

Picha Mei 13 Simba sc Yatamba Kuishangaza Afrika

Thu, 13 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

-wanaoushikilia.

Simba itaikaribisha Dodoma Jiji FC katika mechi ya hatua ya robo fainali itakayochezwa kati ya Mei 25 na 27, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam huku keshokutwa ikishuka ugenini kuwakabili Kaizer Chiefs katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mechi kati ya Kaizer Chiefs dhidi ya Simba itachezwa kwenye Uwanja wa FNB kuanzia saa 1:00 usiku kwa saa za Tanzania.

Gomes ameliambia Nipashe kuwa amefurahishwa na ratiba ya mechi za michuano hiyo na kuitaja Dodoma Jiji ni moja ya timu nzuri hapa nchini, lakini amesisitiza Simba wanalihitaji kombe hilo.

Kocha huyo amesema amefuatilia droo hiyo na wamepangwa kucheza dhidi ya Dodoma Jiji ambayo ni timu nzuri na aliiona kwenye mechi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ilipocheza na Simba.

"Haitokuwa mechi rahisi. Dodoma Jiji ni timu nzuri, nimecheza nayo. Siyo rahisi kuifunga, na kama tukipita hapo nafikiri kwa kiasi kikubwa tutakutana na Azam. Nayo ni timu nzuri na ngumu, niliiona ilipocheza na Yanga na kushinda bao 1-0, lakini nawaamini sana wachezaji wangu. Simba kwa sasa ni timu nzuri na ushahidi kwenye mechi ya FA iliyocheza dhidi ya Kagera Sugar. Ilikuwa mechi nzuri sana," amesema kocha huyo.

Aliongeza wanahitaji kulichukua kombe hilo ili kuendeleza ubora waliouonyesha msimu huu na anaamini uwezo wa kulichukua wanao.

"Ni droo ngumu lakini tunataka kushinda kila kitu, kila kombe msimu huu. Ni muhimu kwetu kama tutashinda Kombe la FA, tutakuwa tumefanya kazi nzuri sana na nawaamini vijana wangu," Gomes amesema.

Kuelekea mchezo wa keshokutwa, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara amesema kikosi chao kiko imara na kila mchezaji ana morali nzuri.

Manara amesema Simba inauwezo wa kufanya vizuri katika mchezo huo na wanaamini wanaweza kupata ushindi ugenini.

"Hatuna majeruhi, hiyo ni faraja kwetu, tuko tayari kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi, tuliwasili hapa Johannesburg salama, maandalizi yako vizuri, timu yetu iliyotangulia imetuandalia mapokezi mazuri, balozi ametupokea vizuri... tunamwomba Mwenyezi Mungu Inshaallah hadi siku ya Jumamosi tusiwe na majeruhi yoyote, tunaweza huenda tukaishangaza Afrika kwa kupata matokeo ugenini," amesema Manara.

Baada ya mchezo huo wa kwanza, Simba itarejea nchini tayari kuwakaribisha Kaizer Chiefs katika mchezo wa marudiano utakaochezwa Mei 22, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Chanzo: ippmedia.com