Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba sasa kambi Ulaya

Mitani Simba Data Mabingwa wa Ligi Kuu Bara Simba

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mabingwa wa Ligi Kuu Bara Simba huenda wakabadili mawazo ya eneo watakaloweka kambi yao ya maandalizi ya msimu, wakifikiria kwenda Ufaransa, ila kutegemea na uamuzi wa Kocha Mkuu wao, Didier Gomes kama atachomoa pendekezo lao la kuweka kambi yao nchini Morocco badala ya Misri.

Awali Simba ilipanga kwenda Misri katika Mji wa Alexandria kutokana na pendekezo la Gomes na fasta mabosi wa klabu hiyo walianza mchakato wa kulikamilisha hilo ikiwemo kuomba visa.

Inaelezwa mabosi hao wa Simba, wamebadili mawazo na wanaweza kuweka kambi Morocco kwani taratibu za kuingia humu si ngumu na kila kitu kinapatikana kwa haraka ikiwemo hoteli, eneo ambalo watafanyia mazoezi mbalimbali na mambo mengine ya msingi. Mabosi hao wa Simba ambalo wamelipanga wakati huu ni kumueleza (Gomes), kuwa upatikanaji wa mahitaji ya msingi, Morocco ni rahisi kuliko kule Misri alipo pendekeza awali.

Katika kipindi cha miaka minne katika kikosi cha Simba tangu kuingia kwa Mwenyekiti wa bodi, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ wamekuwa wakibadilisha nchi mbalimbali kwa ajili ya maandalizi ya msimu.

Mo Dewji ameipeleka Simba, Uturuki, Afrika Kusini mara mbili na awali hii kama si Morocco basi watakwenda Misri na hapo ambacho kinasubiriwa ni maamuzi ya Gomes tu.

Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema maandalizi ya msimu yatafanyika kama ilivyo kawaida yao na hilo linategemea benchi lao la ufundi litakuwa linahitaji eneo gani sahihi.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz