Droo ya CAF kupanga mechi za hatua ya robo fainali imefanyika leo tarehe 30/04/2021 saa 9:00 alasiri mjini Cairo Misri.
Submitted by Tigana Lukinja on Ijumaa , 30th Apr , 2021 Picha ikionesha kombe la mshindi wa michuano ya klabu bingwa Afrika.
Droo iliyokuwa inasubiriwa kwa bashasha kubwa na wadau wa michezo Africa na Duniani kiujumla ambayo iliyohusisha mashindano yote mawili yaliopo chini ya CAF, yaani kombe la shirikisho pamoja na kombe lenye mvuto zaidi la klabu bingwa.
Kwa upande wa kombe la shirikisho, droo imezipanga timu zote 8 katika hatua ya robo fainali kama ifuatavyo 1 Pyramids {Misri }vs Enyimba {Nigeria} 2.Orlando Pirates {A kusini } vs Raja Casablanca { Morocco} 3.Coton Sports { Cameroon} vs ASC Jaaraf {Senegal} 4.CS Sfaxien {Tunisia} vs JS Kabylie {Algeria}
Kwa upande wa kombe la klabu bingwa Africa ambayo Tanzania inawakilishwa na timu ya Simba droo imeshuhudia timu zote 8 zikipangwa kama ipasavyo 1. Simba {Tanzania } vs Kaizer Chiefs {A.kusini} 2.Al Ahly {Misri} vs Mamelod Sundowns { A. kusini} 3 Mc Alger (Algeria} vs Wydad Casablanca { Morocco} 4.CR Belouzidad {Algeria} vs Esperance { Tunisia} Michezo ya klabu bingwa Afrika inataraji kuanza kuchezwa tarehe Mei 14 na 15 kwa michezo ya mkondo wa kwanza ilhali michezo ya mkondo wa pili itachezwa tarehe 21 na 22 Mei, 2021. Kwa ile ya Shirikisho itachezwa tarehe 16 mei kwa ile ya mkondo wa kwanza na mkondo wa pili kuchezwa tarehe 23, 2021.