Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba nguvu zote Ligi Kuu

E2040442eb580570eb01303e788ae901.jpeg Simba nguvu zote Ligi Kuu

Mon, 24 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema licha ya timu yake kuondolewa katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, amefurahishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake na sasa akili yote wameihamishia katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Azam.

Akizungumza baada ya mchezo huo wa marudiano uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salam juzi, Gomes alisema ilikuwa mechi ya jasho na damu, wachezaji walijitoa lakini sasa ni wakati wa kusahau maumivu yaliyopita na akili kuzihamishia katika michezo iliyobakia ya Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na Kombe la Shirikisho la Azam ambalo wako katika hatua ya nane bora.

Simba imeshindwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuondolewa kwa jumla ya mabao 4-3, ikipoteza 4-0 ugenini Afrika Kusini na mechi ya marudiano kushinda 3-0 nyumbani katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Ulikuwa mchezo mzuri kwa pande zote mbili, tulicheza kwa tahadhari kubwa huku tukitengeneza nafasi ambazo baadhi tulizitumia lakini tumeshindwa kufikia malengo yetu kuingia hatua ya nusu fainali.”

“Nawapongeza wachezaji wangu kwa kufuata maelekezo, sasa tunageukia katika michezo ya Ligi na Kombe la Shirikisho ambako naamini tutaenda kufanya vema kutokana na muendelezo wetu mzuri wa matokeo hasa nyumbani.”

“Sasa tunakwenda katika majukumu ya kimkakati kuhakikisha tunatwaa mataji yote yaliyobakia ili tuweze kupata nafasi ya kucheza tena michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema Gomes.

Naye Kocha Mkuu wa Kaizer Chiefs, Gavin Hunt alisema amefurahishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake, japokuwa walifanya makosa ambayo yaliweka rehani nafasi yao ya kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Nilikuwa na presha sana hasa kipindi cha pili wapinzani wetu walikuwa bora nililazimika kufanya baadhi ya mabadiliko ili kupunguza kasi ya mashambulizi, lakini nashukuru nimefuzu hatua ya nusu fainali,” alisema Hunt.

Chanzo: www.habarileo.co.tz