Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba nayo haitanii

32547 Simba+pic Kikosi cha Simba

Thu, 20 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mabingwa wa Soka Tanzania, Simba wameonyesha kuwa wana kikosi kipana baada ya jana kuishinda KMC ya Kinondoni mabao 2-1 katika mchezo mkali wa Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kocha wa timu hiyo, Patrick Aussems aliwapumzisha mastaa wengi wa timu hiyo akiwatumia wachezaji wengi ambao hawapati nafasi mara kwa mara lakini baadaye aliyaingiza majembe yake kipindi cha pili.

Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 30 ikibakia kwenye nafasi yake ya tatu nyuma ya Azam yenye pointi 40 wakati Yanga inaongoza ikiwa na pointi 44. KMC inabakia na pointi zake 21.

Mchezo ulivyokuwa

Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao, alikuwa mshambuliaji wa timu hiyo Adam Salamba ambaye ameendelea kutumia vyema nafasi ya kucheza anayopata mara chache ndani ya kikosi cha Simba baada ya kuipatia bao la kuongoza dakika ya 11. Bao hilo lilitokana na mpira wa krosi uliotokea upande wa winga ya kushoto ambao ulipigwa na Haruna Niyonzima aliyefanya kazi ya ziada kumtoka beki, Kelvin Kijiri wa KMC na kunyunyiza krosi ndogo na Salamba kuunganisha wavuni. Kufungwa kwa bao hilo na Salamba ni kama liliwachochea zaidi Simba kwani dakika tatu baadaye, Said Ndemla aliiandika Simba bao la pili akiunganisha kwa shuti kali pasi ya Mzamiru Yassin. Pamoja na uwanja kuonekana una hali ya utelezi, Simba walionekana kutawala zaidi kulinganisha na KMC. Hata hivyo, wachezaji wa KMC, Salum Chuku, Elias Maguli walibanwa muda wote na mabeki wa Simba chini ya Juuko Murshid na Paul Bukaba.

Pamoja na kosakosa za hapa na pale hadi kumalizika dakika 45 za kwanza, Coulibaly ambaye mchezaji mpya wa timu hiyo, alikonga nyoyo za mashabiki wa timu yake kutokana na kiwango kizuri alichokionyesha kwenye dakika za mwanzoni za mchezo huo. Coulibaly alianzishwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha Simba tangu aliposajiliwa, amekuwa akifanya vizuri katika kukaba na kupandisha mipira mbele kwa haraka kusaidia mashambulizi kwa kupiga krosi za mara kwa mara jambo ambalo limefanya mashabiki kumshangilia mara kwa mara. KMC ilianza kipindi cha pili kwa kufanya mabadiliko, lakini hata hivyo hayakuwa na manufaa kwa timu hiyo.

Kiungo Haruna Niyonzima na Adam Salamba pamoja na Adam Juma walikuwa wakionana vizuri mara kadhaa, lakini hata hivyo mashuti yao ama yalitoka nje au yliokolewa na kipa wa KMC.

Dakika ya 67, James Msuva aliipatia KMC bao baada ya mabeki wa Simba, Murshid na Bukaba kuzubaa kuondosha mpira uliochezwa na kipa Deo Munisi ‘Dida’.

Baada ya bao hilo kocha wa Aussems alimtoa Salamba na kumwingiza Meddie Kagere. Awali Cletous Chama aliingia kuchukua nafasi ya Juma Rashid.



Chanzo: mwananchi.co.tz