Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba na Yanga yamponza mlindalango, Ramadhani Kabwili kuondolewa Ngorongoro Heroes

7402 Kabwili TZW

Fri, 4 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Mlindalango namba moja wa timu ya taifa ya Tanzania kwa vijana waliyo chini ya umri wa miaka 20 Ngorongoro Heroes, Ramadhani Kabwili ameondolewa kwenye timu hiyo ya vijana kwa kushindwa kuripoti kambini mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa watani wa jadi Simba SC na Yanga SC siku ya Jumapili iliyopita.



Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Ammy Ninje amesema kuwa kwakuwa utaratibu haukufuatwa ameamua kumuondoa Kabwili na nafasi yake kuchukuliwa na golikipa kutoka Zanzibar.

Nitaongeza golikipa mwingine kwasababu tuna kutoelewana na Kabwili kwahiyo nimemuacha aendelee na majukumu yake ya Young Africans kwahiyo kuna golikipa anatoka Zanzibar atakuja.

Nikufuata utaratibu niliwapa mapumziko ya siku nne sasa baada ya siku hizo nilikwenda kwenye mechi ya Simba na Yanga nikamuona amekaa kwenye benchi kitu ambacho kilikuw kizuri kwa yeye kupata uzoefu lakini alitakiwa baada ya mechi ajiunge na wenzie kambini kwahiyo hakutokea.

Tuliongeanae Kabwili mimi nampenda kuliko mtu yoyote kwakuwa nimeanza nae kazi toka nipo na mwalimu Mayanga nimefanyanae kazi kwenye CECAFA nampenda sana lakini nadhani hawakufuata utaratibu wa kumrudisha mchezaji kambini ili wamuombe tena na mimi sina pingamizi alipo Kabwiri Yanga ndiyo inamlipa mshahara lakini hapa ni utaifa.

Ngorongoro Heroes kwa sasa ipo kambini kujiwinda dhidi ya timu ya taifa ya MaliĀ  siku ya Jumapili ya Mei 13 mwaka huu 2018 kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam ukiwa ni wa raundi ya pili kufuzu fainaliĀ  za vijana Afrika.

Loading...
Chanzo: bongo5.com