Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba mikononi mwa mabingwa 6

33867 Pic+sim Tanzania Web Photo

Fri, 28 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Timu tatu kati ya saba zilizowahi kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika miaka ya nyuma zinaweza kupangwa kundi moja na Simba katika droo itakayochezeshwa jijini Cairo, saa tatu zijazo. Kupangwa katika vyungu tofauti vya droo hiyo itakayochezeshwa katika Hoteli ya kifahari ya Al Qahira Ballroom (Nile Ritz-Carlton) kuanzia saa 12.00 kwa saa za Misri sawa na saa 1 usiku kwa muda wa Tanzania, kunaleta uwezekano wa wawakilishi hao wa Tanzania kupangwa na miongoni mwa timu hizo. Simba iliyo katika chungu C, haina uwezekano wa kukutana na timu tatu tu katika hatua ya makundi ambazo ni CS Constantine ya Algeria, Orlando Pirates ya Afrika Kusini na Asec Mimosas ya Ivory Coast ambazo imepangwa nazo chungu kimoja. Simba haina namna zaidi ya kukutana na timu mojawapo kati ya Al-Ahly ya Misri iliyotwaa ubingwa wa mashindano hayo mara nane (8), TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) iliyotwaa ubingwa huo mara tano (5), Eaperance iliyochukua mara tatu (3) na Wydad Casablanca ambayo imeibuka bingwa mara mbili (2) ambazo zipo chungu cha kwanza.

Mabingwa wengine ambao Simba inaweza kukutana nao ni Mamelodi Sundowns iliyochukua mara moja sawa na AS Vita ya DRC na Club Africain ya Tunisia ambazo zipo chungu cha pili sawa na Horoya ya Guinea. Timu nyingine iliyowahi kutwaa ubingwa ambayo Simba wanaweza kukutana nayo ni Ismaily ya Misri ambayo yenyewe ipo chungu cha nne

Chanzo: mwananchi.co.tz