Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba mambo yake safi Afrika Kusini

10c83122fa59bebeff9851dab1a0ab13.jpeg Simba mambo yake safi Afrika Kusini

Wed, 12 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MENEJA wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema wako tayari kupambana na kupata pointi tatu kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kazier Chiefs baada ya kuwasili salama Afrika Kusini jana.

Akizungumza kwa njia ya mtandano na gazeti hili Rweyemamu alisema mchezo huo utachezwa Jumamosi saa 12:00 kwa saa za Afrika Kusini na kwa Tanzania itakuwa saa 1:00 jioni.

“Tunashukuru tumefika salama, tunaendelea na maandalizi ya mchezo, muhimu ni kupata pointi tatu,” alisema Rweyemamu.

Naye nahodha John Bocco alisema wanaendelea na maandalizi na wanaamini watapata ushindi katika mchezo huo wa robo fainali.

“Tunaamini tutapata matokeo mazuri,” alisema Bocco kwa kifupi baada ya kuwasili Afrika Kusini jana.

Mchezo huo siyo mwepesi kwa sababu Kaizer Chiefs wanacheza kwa kasi, wana washambuliaji wenye nguvu na ubunifu lakini Simba wana faida ya kufahamu namna ya kucheza na timu zinazotoka Jangwa la Sahara.

Kazier Chief kwenye ligi yao hawako vizurikwa sababu nguvu zao wamewekeza katika Ligi ya Mabingwa Afrika hivyo Simba wasiwachukulie kama mchezo mwepesi wacheze kwa kiwango kile kile kama walivyocheza kwenye mechi nyingine za kimataifa, wasifanye makosa.

Simba ilifuzu robo fainali baada ya kuongoza Kundi A ikifuatiwa na Al Ahly ya Misri huku timu za AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia Congo na Al Merreikh ya Sudan zikishindwa kufuzu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz