Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba makali mwanzo mwisho

E746eed247210ca3d3cbfc85b528190a Simba makali mwanzo mwisho

Tue, 21 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KOCHA wa Simba Sven Vandenbroeck amepania kushinda michezo miwili iliyosalia, ukiwemo dhidi ya Coastal Union unaotarajiwa kuchezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga, ili kukamilisha ratiba ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa mwaka 2019/2020.

Simba ambao hadi sasa wamekwishatangazwa mabingwa wa ligi na kutete kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kufikisha pointi ambazo haziwezi kufikiwa na timu zingine kati ya 20 zinazoshiriki ligi hiyo inayoelekea ukingoni.

Akizungumza Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita,baada ya kikosi hicho kuibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Alliance FC kwenye mchezo wa Ligi hiyo uliofanyika juzi, kwenye Uwanja wa Taifa, Sven alisema, pamoja na kuwa mabingwa bado wana kazi ya kuhakikisha wanashinda mechi zote zilizobaki.

“Bado tunajukumu la kupata ushindi kwenye mechi zote mbili zilizosalia kama tuliopata leo (juzi) dhidi ya Alliance kuendelea kuwapa burudani mashabiki wetu ambao muda wote wamekuwa wakituunga mkono,” alisema Sven.

Sven aliongeza kwamba ushindi huo ulikuwa maalumu kwa kuwaonesha mashabiki wa Dar es Salaam taji la ubingwa wa ligi hiyo walichokabidhiwa mkoani Lindi walipocheza dhidi ya Namungo FC na kutoka suluhu.

Aidha, Sven hakusita kuzungumzia kiwango duni kilichooneshwa na nyota wake kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mbao FC waliopoteza kwa mabao 3-2, ambapo alidai kuwa wachezaji wake waliwabeza wapinzani wao.

Alisema mchezo wa mpira una mambo mengi anajua siku haziwezi kufanana, lakini amewaambia wachezaji wake kupambana katika mechi mbili zilizobaki ili kumaliza kwa kishindo ligi hiyo pamoja na fainali ya Kombe la FA.

Mechi hiyo ya fainali itawakutanisha Simba dhidi ya Namungo mechi iliyopangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga mkoani Rukwa Agosti 2.

Chanzo: habarileo.co.tz