Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kuvaana na Ulimwengu

33885 Pic+dro Tanzania Web Photo

Fri, 28 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Simba itakutana na mshambuliaji wa Kitanzania Thomas Ulimwengu katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayoanza mwezi ujao. Katika droo inayochezeshwa huko Cairo Misri usiku huu, Simba imepangwa kundi D sambamba na JS Saoura ya Algeria ambayo imemsajili mshambuliaji huyo siku chache zilizopita. Ulimwengu amejiunga na Saoura akiwa mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake na All Hilal ya Sudan miezi michache iliyopita. Hii sio mara ya kwanza kwa Ulimwengu kukutana na timu ya Tanzania kwenye mashindano ya klabu Afrika kwani mwaka 2016 alikutana mara mbili na Yanga kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Chanzo: mwananchi.co.tz