Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kurejesha heshima ya Boban

42132 Pic+boban Simba kurejesha heshima ya Boban

Mon, 18 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

WATAALAMU wa soka nchini, wamemchambua kiungo wa Yanga, Haruna Moshi ‘Boban’ atakayecheza dhidi ya timu yake ya zamani ya Simba kwa mara ya kwanza katika derby na kudai ndilo litakalomrejeshea heshima mbele ya wadau wa soka.

Boban alipata umarufu mkubwa akiwa na Simba, ambapo katika dabi ya leo atakuwa mpinzani wa timu hiyo akiwa na Yanga, kitendo kilichoibua mjadala mzito dhidi yake, huku wakimtolea mfano wa kumpiku Haruna Niyonzima.

Mchambuzi Ally Mayay alisema umaarufu wa Boban aliupata akiwa Simba na leo atacheza kwa mara ya kwanza katika derby ya 2018/19 akiwa upande wa Yanga, alimshauri kufanya mambo mawili muhimu kuwa kiongozi wa wenzake namna ya kucheza mipira ya utulivu na nidhamu.

Mayay alisema mechi zilizopita Boban mchango wake ndani ya Yanga una asilimia 70, akitaja sababu za kutokufikisha 100 kwamba inatokana aina ya uchezaji wa timu nzima ulivyo unaomfanya wasiojua soka wamuone wakawaida.

“Mechi ya leo naitazama kama ya kurudisha ufalme wa Boban, sababu kubwa Simba inacheza kwa kumiliki mipira na Boban ni mtu wa kukaa na mpira mguuni na hana papara ya pasi, hilo ndilo litafanya awe msaada mkubwa kwa timu yake,” alisema.

Naye kocha wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni alisema Boban ana kipaji cha kuzaliwa na ikitokea leo kauamulia mchezo basi anaweza akawashangaza wengi na kurudi midomoni mwa wadau wa soka nchini.

“Boban ana kitu kimoja siku akiamua kwamba anafanya zaidi ya kile alichoelekezwa mazoezini basi anashangazaga wengi, ana kipaji cha aina yake ambacho hakichoshi kumuangalia anapokuwa kwenye kiwango,leo mguu wake ukiamka na kazi basi atafanya kitu cha tofauti sana, ila Simba ushindi lazima.

“Pia anatakiwa awe na dhamira ya kutaka kuandika rekodi ya aina yake kwenye dabi ya leo kitu hicho kitamtofautisha na Niyonzima ambaye alicheza kwa muda mrefu Yanga alipokuja Simba alishindwa kutamba kwenye mchezo wa watani,” alisema.



Chanzo: mwananchi.co.tz