Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kupeleka kombe Kigoma

A460ebf284353c779d255b8ecd594ade Simba kupeleka kombe Kigoma

Thu, 8 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MENEJA wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema wamepanga kuwapelekea zawadi ya kombe la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mashabiki wao wa Kigoma, wakati timu yao itakapo kwenda kucheza mechi ya fainali ya Kombe la FA dhidi ya Yanga.

Simba na Yanga zitakutana Julai 25 kwenye dimba la Lake Tanganyika Kigoma katika mchezo wa fainali ya Kombe la FA ambao unatarajiwa kuhudhuriwa na mashabiki wengi kutokana na timu hizo kukutana kwa mara ya kwanza kwenye uwanja huo.

Rweyemamu alisema ili kutimiza lengo lao wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi katika mechi zao zote tatu za ligi zilizobaki ili kutwaa taji hilo ambalo litakuwa ni la nne mfululizo.

“Tunasafari ya Kigoma na huko tuna mashabiki wengi na vibaya zaidi hatujakwenda siku nyingi, sasa kwakua tuna mechi ya fainali dhidi ya watani zetu Yanga, tumepanga kuwapelekea zawadi ya kombe la ubingwa wa Ligi Kuu mashabiki wetu halafu tuwape burudani kwa soka safi na taji jingine la FA, “ alisema.

Rweyemamu alisema anatambua ugumu wa kupata ushindi katika mechi zao tatu zilizobaki za ligi, lakini anaamini watafanikisha lengo lao na hiyo inatokana na uimara wa kikosi chao ikilinganishwa na wapinzani wao.

Alisema watafanya kila linalowezekana ili kutetea taji lao na kazi yao wameiacha kwa wachezaji ili kuthibitisha ubora wao kwa kupata ushindi bila kujali ukubwa wa timu ambazo watacheza nazo.

Rweyemamu alisema kipigo dhidi ya watani zao Yanga, kimewazindua na kuwalazimu kufuta mapumziko ya baada ya kila wanapocheza mechi ya ligi kama ilivyo kawaida yao, lengo ni kuhakikisha wanaongeza umakini na kufanya vizuri kwenye mechi hizo zilizobakia.

Meneja huyo alisema wanachokifanya hivi sasa ni kuwajenga wachezaji wao kisaikolojia ili mawazo yao yafikirie kwenye mechi hizo, ambazo zinawakabili ambazo wamezipa uzito mkubwa ili kuhakikisha wanatimiza malengo yao ambayo walijipangia mwanzoni mwa msimu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz