Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kupata baraka Dodoma kabla kutafuta pointi tatu za Singida United

7720 Simbaaa.png TZW

Thu, 10 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Klabu ya Simba imesema kuwa kabla ya kuwakabili wapinzani wao timu ya Singida United kwenye mchezo utakao amua kuwa bingwa rasmi wa ligi kuu soka Tanzania Bara msimu huu kama watashinda basi watapita mkoano Dodoma na kuweka kambi ya muda.



Taarifa rasmi kutoka ndani ya uongozi wa timu hiyo imesema kuwa Simba tayari imeshaondoka jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo na ipo njiani kuelekea mkoani Dodoma kabla ya kucheza na Singida United.

Meneja wa kikosi cha Simba Richard Robert alisema ‘Tumeanza safari yetu kuelekea Singida Kwa ajili ya mchezo unaofuata dhidi ya Singida Utd, safari yetu tutapitia mkoani Dodoma na kuweka kambi ya muda kabla ya kwenda Singida’

Klabu ya Simba ambayo inahaha kuhakikisha inatwaa taji la ligi kuu msimu baada ya kulikosa kwa miaka mitano itahitaji ushindi kwenye mchezo wake na Singida United siku ya Jumapili ili kujihakikishia inatawazwa kuwa mabingwa rasmi msimu huu baada ya kuwa na jumla ya pointi 65 kwenye msimamo.



Wekundu wa msimbazi Simba wametwaa ubingwa huu mara ya mwisho ikiwa ni msimu wa mwaka 2011/12 kisha Yanga msimu wa mwaka 2012/13 na Azam FC mwaka 2013/14 kisha Yanga ikatwaa tena mfululizo msimu wa mwaka 2014/15, 2015/16 na 2016/17 na sasa vijana wa Simba wanasema Simba yao, mwaka wao.

Loading...
Chanzo: bongo5.com