Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kumpa nafasi Niyonzima ajieleze

9986 PIC+NIYONIMA TanzaniaWeb

Sat, 4 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.KLABU ya Simba imesema itampa nafasi pili, Haruna Niyonzima ambaye kwa sasa yuko nchini Rwanda alikokwenda kwa ajili ya kujitibia.

Kaimu Rais wa Simba, Abdallah Salim 'TryAgain' amesema Haruna aliomba kwenda kwao kwa ajili ya kujiangalizia baada ya ligi kumalizika, na akatoa maagizo kwamba alipiwe viza yake.

"Tumemlipia viza ya kwenda Uturuki, lakini hakutokea, ruhusa yake ilikuwa inamalizika Julai 20, lakini sasa hatutaki kusema lolote, kikubwa tutamuita kama uongozi kwa ajili ya kumsikliza upande wake kama ana cha kusema," amesema.

Amesema: “Tarehe ambayo alitakiwa kurudi Haruna ilikuwa ni Julai 20 na kama ilivyokuwa mwaka jana alikosa pre-season hata performance yake haikuwa nzuri kwa sababu ya kukosa pre-season na kukaa pamoja na wenzake.”

“Mwaka huu tena anakutana na tatizo hilo hilo, sisi kama uongozi tunajaribu kuangalia kwa nini Haruna hajajiunga na timu kwa ajili ya pre-season japokuwa na yeye tutampa nafasi ya kujieleza.”

“Zipo taratibu na namna ya kufanya, kama ni makosa basi tutamwadhibu kwa mujibu wa taratibu zetulakini tutampa nafasi ya kujieleza kwa nini hajajiunga na timu.”

“Inawezekana ikawa ni tabia yake lakini na sisi kama klabu tuna tabia yetu kwa hiyo hatuwezi kuiga tabia yake. Kama amekosea zipo taratibu za kuchukua, yule ni mchezaji inawezekana ana jambo linamsumbua tutamwita tutamsikiliza halafu tutaona ni kitu gani cha kufanya.”

 

Chanzo: mwananchi.co.tz