Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kufichwa mbali Botswana, Morrison, Bocco wavishwa mabomu

Simbasctanzania Simba kufichwa mbali Botswana, Morrison, Bocco wavishwa mabomu

Sat, 16 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

SIMBA inapaa leo jioni kwenda Botswana kutekeleza majukumu mazito ya kimataifa dhidi ya Jwaneng Galaxy huku mastaa wawili wakipewa kazi ya kusimamia shoo hiyo.

Wekundu hao wanakiwasha saa 10:00 jioni Jumapili kwenye mechi muhimu ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo akipata matokeo mazuri nyumbani na ugenini anaingia makundi.

Kwa mujibu wa mazoezi ya juzi na jana, uwezekano wa Chris Mugalu kucheza haupo, hivyo John Bocco na Benard Morrison wamevishwa mabomu ya maangamini kuwainua Watanzania na mashabiki wa Simba Jumapili.

Mwanaspoti linajua kuwa mshambuliaji tegemeo wa wekundu wa msimbazi, Mugalu ana majeruhi baada ya kuumia kwenye mazoezi kuelekea mchezo wa ligi dhidi ya Biashara United ambao ulimalizika kwa suluhu.

Mugalu hakuhusika katika mechi hiyo na alirejea uwanjani kwenye mechi ya Dodoma Jiji iliyomalizika kwa Simba kushinda 1-0 akitoa asisti kwa ya bao pekee la timu hiyo lililowekwa kambani na Meddie Kagere dakika ya 70 licha ya kwamba alikuwa hajapona vizuri.

Baada ya mechi hiyo kumalizika, Simba ilirejea Dar es Salaam na Mugalu kupewa mapumziko akiendelea kuuguza jereha lake huku Kagere na wengine wakienda kwenye timu zao za taifa na hadi jana Mugalu alikuwa hajajiunga na timu mazoezini hivyo kumlazimu kocha mkuu, Didier Gomes kuwapa majukumu maalumu Bocco na Morrison ambao wako moto kwelikweli na wenyewe.

Mwanaspoti limekuwa ‘live’ mazoezini kwa Simba kila Siku na limeshuhudia Morrison na Bocco wakipewa kazi ya kuifungia mabao timu hiyo huku wakisaidiana na wachezaji wengine na wamefanya kazi hiyo kwa ufasaha jambo linalotia matumaini safari ya makundi inawahusu Simba.

Bocco na Morrison wananafasi kubwa ya kuanza wakisaidiana na Hassan Dilunga katika eneo la ushambuliaji.

Rally Bwalya, Taddeo Lwanga na Sadio Kanoute watacheza eneo la kiungo kama kawaida huku Mohamed Hussein, Shomari Kapombe, Kennedy Juma na Pascal Wawa wakitarajiwa Onyango eneo la beki na Manula atasimama langoni.

Hata hivyo, kulingana na mazoezi yanavyoonekana huenda washambuliaji Kibu Denis na Yusuph Mhilu wakawa sehemu ya mechi hiyo wakitokea Sub, kwani mazoezini wamekuwa wakikiwasha balaa.

Akizungumzia mchezo huo, kocha Gomes ameeleza kuwa; “Tuko vizuri, nimewafuatilia Galaxy wako vizuri pia lakini kwakuwa tunataka kufika mbali msimu huu kwenye Ligi ya Mabingwa basi hatunabudi kushinda mechi hiyo ugenini,” alisema Gomes na kuongeza;

“Naweza kufanya mabadiliko kadhaa ya kikosi kitakachoanza kutokana na hali ya timu kwa sasa lakini mchezaji atakayepata nafasi ni yule atakayeonesha ubora na kiwango bora mazoezini,” alisema Gomes ambaye Galaxy wamepanga kuwachezesha saa 9 za kule kwao ambapo ni jua kiasi.

Mmoja wa viongozi wa Simba aliliambia Mwanaspoti jana kwamba wamedhibiti mianya yote ya hujuma Botswana na wameafikiana kwamba timu hiyo ifikie nje kidogo ya mji lakini siyo mbali na Uwanja wa mechi ili kuzuia hujuma.

Alisisitiza ndani ya kambi hiyo kutakuwa pia na ulinzi mkali kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz