Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kama Yanga yatinga robo fainali ASFC

Morrison Pc Data 79767449

Sun, 2 May 2021 Chanzo: eatv.tv

Timu ya soka ya Simba imekuwa timu ya saba kufuzu hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho la Azam baada ya kuifunga Kagera Sugar 2-1 katika mechi iliyopigwa katika uwanja wa hayati Benjamin Mkapa jijini Dar-es-salaam jumamosi hii .

Kagera ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli kunako dakika ya 45 kipindi cha kwanza lililowekwa wavuni na chipukizi Eric Mwijage kwa kichwa akiunganisha krosi maridhawa ya winga Vitalisi Mayanga ambaye alikuwa na siku nzuri sana mchezoni.

Simba ambao ni mabingwa watetezi wa kombe hili walibadili upepo zaidi katika kipindi cha pili, baada ya kufanya mabadiliko kumuingiza Bernard Morrison hatimaye kufunga goli na kusaidia kupatikana kwa goli la pili lililofungwa na Meddie Kagere.

Kwa ushindi huo Simba inaungana na timu nyingine 6 kufuzu hatua ya robo fainali akiwemo, mtani wake wa jadi Yanga ambaye alifuzu baada ya kumfunga kwa mbinde Tanzania Prisons 1-0 siku ya ijumaa katika uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga.

Timu zilizofuzu hadi sasa ni Rhino Rangers ya Tabora, Mwadui ,Biashara United, Azam, Dodoma jiji, Simba na Yanga, huku ikisaliwa na mchezo moja katika hatua hii ya 16 bora kati ya JKT Tanzania dhidi ya Namungo unaofanyika leo,

Droo ya robo fainali itachezeshwa baadaye ambapo huwenda Yanga na Simba wakakutana katika hatua hii, kwa mara ya mwisho kukutana katika kombe hili ilikuwa nusu fainali ya msimu uliopita ambapo Yanga walikubali kichapo cha bao 4-1

Chanzo: eatv.tv