Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

''Simba itatawala kwa miaka 15 hadi 20''Morrison

Bm 2 ''Simba itatawala kwa miaka 15 hadi 20''Morrison

Sun, 23 May 2021 Chanzo: eatv.tv

Mshambuliaji wa Klabu ya Simba, Benard Morrison amesema anayo furaha kubwa ya kuitumikia miamba hiyo ya soka hapa nchini na imani yake kubwa ni kwamba wekundu hao wa msimbazi watatawala soka la nchi kwa miaka mingi ijayo.

Submitted by George David on Jumapili , 23rd Mei , 2021 Mshambuliaji wa Simba, Benard Morrison akifurahia jambo mara baada ya kikosi chake kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania bara msimu uliopita.

Kauli ya Morrison inakuja muda mchache baada ya Simba kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini licha ya ushindi wa bao 3-0 walioupata jana kwwenye dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam lakini haukutosha kuwavusha kwenda nusu fainali kutokana na matokeo ya jumla ambayo yamewafanya waondolewe kwa bao 4-3.

''Ninajivunia sana kuvaa jezi hii ya Simba, sababu ninafuraha.Simba huwezi ilinganisha na Klabu yoyote Tanzania.Tutashinda makombe yote  yaliyobaki.Timu zingine haziwezi kucheza kimataifa bila Simba.Simba itaiwakilisha Tanzania kwa miaka 15 hadi 20 ijayo''Benard Morrison.

Morrison alijiunga na Simba akitokea Yanga uhamisho ambao ulizua mtafaruku mkubwa ikidaiwa kwamba nyota huyo alikuwa na mkataba na waajiri wake wa zamani.

Simba ndio mabingwa watetezi wa VPL na wapo katika nafasi nzuri ya kutetea taji lao wakiwa na alama 61 sawa na Yanga lakini wao wakiwa na faida ya michezo ambayo hawajacheza.

Vilevile Simba ndio mabingwa watetezi wa Azam Sports Federation Cup na wapo katika hatua ya robo fainali ambayo wataumana na Dodoma Jiji na iwapo watafuzu wataumana na mshindi kati ya Azam na Rhino Rangers na iwapo watashinda watatinga fainali.

kwa kusikia kwa kina alichokizungumza Morrison tazama video hapo juu .

Chanzo: eatv.tv