Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba imeiumiza TFF, Yanga,Azam wabebeshwa mzigo

73267 Simba+caf+pic

Wed, 28 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kanda ya Dar es Salaam imeonyesha kuumizwa na hatua ya kutolewa kwa klabu za Simba na KMC katika mashindano ya CAF.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kanda ya Dar es Salaam kutoka TFF, Lameck Nyambaya alisema walitarajia makubwa katika klabu zilizokuwa zikishiriki msimu huu.

Nyambaya alisema baada ya Simba kutolewa Ligi ya Mabingwa Afrika huku KMC ikitolewa Shirikisho hawakutarajia timu hizo kutolewa mapema.

Kigogo huyo alisema kufuatia mafanikio ya Simba katika msimu uliopita na usajili walioufanya walitegemea timu nyingi za Tanzania kutinga hatua ya makundi na kwamba hatua ya kutolewa imewashtua kuwataka kukaa chini kujipanga vyema.

Aidha Nyambaya alisema kwasasa TFF na kanda yao wanaelekeza nguvu zao kwa Yanga na Azam FC zilizosalia kuhakikisha nazo hazifanyi makosa.

Alisema tayari wameanza vikao vya kutaka kuhakikisha timu hizo zinafanya kweli katika mechi zao zijazo ili kutopoteza nafasi ya ongezeko la timu katika mashindano hayo.

Pia Soma

 

Chanzo: mwananchi.co.tz