Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba haina kulala

70888 Pic+simba

Mon, 12 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KIKOSI cha Simba jana Jumamosi jioni kilicheza mechi ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo nchini Msumbiji na fasta kikarejea nchini na asubuhi wanaendelea na mazoezi kujiandaa na mechi yao ya Ngao ya Jamii ya wikiendi ijayo na ile ya marudiano ya CAF.

Mara baada ya mchezo huo Simba walirudi nchini na kufika saa 6 :00  usiku huku baadhi ya wachezaji wakienda kambini na wengine majumbani kwao.

Kocha wa Simba, Patrick Aussems katika kuhakisha kikosi hiko hakifanyi mzaha mapema asubuhi ya leo walifanya mazoezi katika uwanja Gymkhana.

Mazoezi hayo walianza saa 10:30 asbh huku wakiwa katika makundi mawili tofauti.

Kundi la kwanza lilikuwa wale wachezaji waliocheza katika mechi ya jana na walifanya mazoezi pekee yao na muda mwingi wakiwa wananyoosha viungo.

Kundi la pili walikuwa wale wachezaji ambao hawakucheza na wengine hawakusafiri na timu na walikuwa wakifanya mazoezi ya kukimbia uwanja mzima.

Pia Soma

Mpaka sasa mazoezi bado yanaendelea.

Chanzo: mwananchi.co.tz