Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba haikamatiki

Picha Juni 04 Simba haikamatiki

Fri, 4 Jun 2021 Chanzo: ippmedia.com

Hata hivyo wenyeji Ruvu Shooting ambao jana waliuteua Uwanja wa CCM Kirumba kuwa nyumbani ilipoteza wachezaji wawili dakika za mwisho kwa kuonyeshwa kadi nyekundu.

Nahodha wa Wekundu wa Msimbazi, Bocco, sasa amefikisha mabao 13, moja nyuma ya kinara wa mabao kwenye ligi hiyo, mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube ambaye ametikisa nyavu mara 14.

Bocco amefunga mabao saba katika mechi nne mfululizo ambazo amecheza. Mabao mawili alifunga kwenye mechi dhidi ya Kaizer Chiefs kwenye michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa, mawili kwenye mechi ya Kombe la FA dhidi ya Dodoma Jiji, moja dhidi ya Namungo katika mechi nyingine ya kiporo.

Kwenye mechi hiyo, Ruvu Shooting ilianza kucheza pungufu kuanzia dakika ya 71, baada ya Juma Nyosso kumpiga ngumi beki wa Simba, Shomari Kapombe huku dakika tatu kabla mechi kumalizika, golikipa Abdallah Rashid naye alizawadiwa kadi nyekundu na mwamuzi, Emmanuel Mwandembwa kwa kumwangusha, Bernard Morrison ndani ya eneo la hatari na kusababisha penalti iliyoipatia Simba bao la tatu.

Rally Bwalya, nusura alipatie Simba bao lingine akiwa katika eneo la hatari baada ya kuachia kombora kali la juu, lakini kipa Rashid aliruka na kuupiga ngumi mpira huo, ukatoka nje ya kuwa kona ambayo ndiyo iliyozaa bao.

Alikuwa ni Bocco dakika ya 17, aliyefunga kona hiyo fupi iliyopigwa na Bwalya kwa Miquissone ambaye alipiga krosi ya chini iliyoguswa na mfungaji na kumpoteza maboya kipa, ukajaa wavuni.

Edward Charles alimshughulisha Manula dakika ya 28, akiwa umbali ya mita 35 hivi, aliachia mkwaju mkali ambao kipa wa Simba aliruka juu kama nyani na kuukamata.

Kipindi cha pili Ruvu ilianza mechi hiyo kwa kasi na kufanya mashabulizi makali kwenye lango la Simba, lakini ilijikuta ikifunga bao lililotokana na shambulio la kushtukiza.

Alikuwa ni Morrison aliyeingia kuchukua nafasi ya Hassan Dilunga, aliyepata pasi ndefu akakimbia nayo kabla ya kupiga krosi iliyomkuta Chris Mugalu dakika ya 61, akaujaza wavuni na kuifungia Simba bao la pili.

Kuingia kwa bao hilo kulionekana kuwachanganya wachezaji wa Ruvu Shooting na kuanza kucheza kwa kutumia nguvu zaidi kuliko akili kiasi cha kufanya makosa mengi yaliyowagharimu.

Kadi nyekundu ya Nyosso, ilisababisha Kocha, Boniface Mkwasa, kumtoa Zuberi Dabi na kumwingiza, Frank Ikobela ili kuongeza nguvu, lakini haikusaidia hadi iliporuhusu bao la tatu.

Alikuwa ni Morrison tena alipompiga chenga ya kifua kipa, Rashid kabla ya kumwangusha na kusababisha kadi hiyo iliyosababisha penalti ambayo ilifungwa na Bocco, golini akiwa kipa mwingine chaguo la pili, Bidii Hussein.

Kwa matokeo hayo, Simba sasa imefikisha ya pointi 67, ikiwa bado ina viporo viwili mkononi ikifuatiwa na Yanga yenye pointi pointi 61 baada ya kucheza mechi 29.

Wakati huo huo Spika wa Bunge, Job Ndungai, amesema sasa hivi ni mwendo wa tatu tatu kuelekea Julai 3, mwaka huu ambapo watani wa jadi watakutana katika mechi ya kiporo ya Ligi Kuu Bara.

Chanzo: ippmedia.com