Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba full mzuka

Simba full mzuka

Mon, 11 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KAMA wewe ni shabiki wa Simba, usiwe na presha. Unachotakiwa kukifanya kwa leo ni kusubiri usiku uingie ukae mbele ya runinga yako, kisha kulicheki chama likiliamsha dude ugenini.

Kama glasi ya kinywaji chochote we kigide kwa raha zako, kwani vile kila kitu kule Algeria kipo vizuri na Mwarabu atapigwa kwao. Ndio, haya sio maneno ya Mwanaspoti bali ni kauli ya Kocha Patrick Aussems na wasaidizi wake, baada ya kufanya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya JS Saoura.

Simba ipo ugenini mjini Bechar kuvaana na JSS katika mechi ya Kundi D ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Agosti 20, 1955 huku ikibebwa na rekodi tamu za mechi za hivi karibuni.

Kocha Aussems aliliambia Mwanaspoti, ni kweli mchezo wa leo atawakosa nyota wake watatu muhimu kikosini akiwamo Emmanuel Okwi, Juuko Murshid na Erasto Nyoni, lakini tayari wabadala wake wapo tayari kulianzisha ugenini na kuwaomba mashabiki kuiombea itoke salama Algeria.

“Simba ina wachezaji wengi wenye uwezo kukosekana kwa hawa bado hakuwezi kuwa tatizo kwetu na tunajua tunakutana na timu iliyobadilika, lakini tumejiandaa kupata ushindi,” alisema Aussems.

Licha ya Mbelgiji huyo kutoanika wabadala wa kina Okwi, laki Mwanaspoti linafahamu nafasi ya Juuko imezibwa na Paul Bukaba, huku pale kwa Okwi ameingia Hassan Dilunga ambao wataungana na kina Aishi Manula, Zana Coulibaly, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Pascal Wawa, James Kotei, Jonas Mkude, Clatous Chama, John Bocco na Meddie Kagere.

Wachezaji wa saba wa akiba watakaokuwa benchi leo ni Deo Munishi ‘Dida’, Asante Kwasi, Rashid Juma, Adam Salamba, Haruna Niyonzima, Mzamiru Yassin na Nicholas Gyan, huku Mohammed Ibrahim na straika chipuklizi Abdul Selemani wenyewe watakuwa jukwaani.

Kikosi hicho cha Simba jana saa 5:00 asubuhi kilisafiri hadi Bechar ikitokea Algiers ilipokaa kwa siku mbili na kujifua, ikiwa na matumaini makubwa ya kupata ushindi kwenye mchezo huo utakaochezwa kuanzia saa 4 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

MKWANJA TISHIO

Nusanusa ya Mwanaspoti ilipata taarifa nyota hao tayari wameshawekewa mezani Sh 100 milioni endapo watapata ushindi katika mchezo huo watachukua na kugawana mara tu wakifika nchini kila mchezaji atachukua mkwanja wake.

Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi Simba Salim Abdallah ‘Try Again’ alikaririwa na gazeti hili jana akisema hakuna mechi ambayo wachezaji wao wanacheza na wakashinda bila ya kuchukua posho ingawa huwa zinatofautiana na kulingana na ukubwa wa mchezo wenyewe.

“Si vyema kuweka wazi lakini kila mechi ambayo unaona Simba wanaondoka na ushindi ujue wachezaji wanapewa posho nje ya mishahara yao na hata katika mechi na JSS itakuwa hivyo hivyo,” alisema Try Again.

REKODI TAMU

Kiu ya kufuzu hatua ya Robo Fainali, hamu ya kufuta uteja mbele ya timu kutoka Kaskazini mwa Afrika pindi inapocheza ugenini pamoja na shabaha ya kuondoa jinamizi la aibu waliyoipata kwenye michezo miwili ya ugenini iliyopita, itakayoifanya Simba iingie kivingine kwenye mchezo wa leo.

Wakiwa nafasi ya pili kundini na pointi sita, Simba wanashuka dimbani leo wakitambua fika kuwa ushindi wa ugenini utawaweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali.

Ushindi utawafanya wafikishe pointi tisa ambazo zitawapunguzia mzigo na kuhitajika kupata sare tu kwenye mechi ya mwisho ili wasonge mbele. Hata hivyo wanaweza kufuzu moja kwa moja iwapo AS Vita yenyewe itapoteza nyumbani mbele ya Al Ahly.

Lakini ukiondoa hilo, Simba ina deni la kuhakikisha inamaliza historia mbaya ya kutopata ushindi ugenini dhidi ya timu kutoka Kaskazini mwa Afrika zinazozungumza lugha ya Kiarabu

Katika mashindano mbalimbali ya Afrika kwa ngazi ya klabu, Simba imekutana na timu kutoka Mataifa ya Kiarabu mara 11 ugenini ambapo kati ya hizo mechi 10 ilipoteza na moja ikatoka sare.

Rekodi hiyo inachagizwa na kipigo cha mabao 5-0 na Al Ahly jijini Alexandria katika mechi ya raundi ya tatu ya kundi lao msimu huu.

Simba inaingia wakiwa sawa kisaikolojia kutokana na mwendelezo wa matokeo mazuri ambayo wamekuwa wakiyapata katika mechi za mashindano, wameshinda tano mfululizo, wakifunga mabao 12 na kufungwa mara mbili. Saoura katika mechi zao tano wameibuka na ushindi mara tatu, sare moja na kupoteza moja, huku wakifunga mabao manne.

Chanzo: mwananchi.co.tz