Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Yaichapa Kagera Sugar Kibabe

SIMBA 6?fit=1080%2C719&ssl=1 Simba Yaichapa Kagera Sugar Kibabe

Sun, 2 May 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) maarufu Kombe la FA, Simba SC, jana walijikatia tiketi ya kufuzu robo fainali ya michuano hiyo baada ya kuichapa Kagera Sugar mabao 2-1, mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

Katika mchezo huo ulioanza saa 1:00 usiku, Kagera Sugar walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Erick Mwijage aliyefunga kwa kichwa dakika ya 45 na timu hizo kwenda mapumziko matokeo yakiwa Simba 0-1 Kagera.

Simba imetinga hatua ya robo fainali ikiungana na Rhino Rangers, Biashara United, Azam, Mwadui, Yanga na Dodoma Jiji, huku akisubiriwa mshindi wa mchezo wa leo kati ya JKT Tanzania na Namungo ili kuhitimisha hatua hiyo kabla ya kwenda robo Fainali.

Chanzo: globalpublishers.co.tz