Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Tanzania mambo ni moto shangwe kila kona

70183 Simbasimba+pic

Tue, 6 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Tawi la Simba Kasi, lililopo Temeke jijini Dar es Salaam, mambo ni moto asikuambie mtu, walianza kukiamsha jana kuelekea kuhitimisha siku yao muhimu leo 'Simba Day', kwenye Uwanja wa Taifa.

Katika pitapita mtaani Mwanaspoti, lilikutana na tawi la Simba Kasi lililoanza kufanya maandalizi ya Simba Day tangu jana Jumatatu ambapo leo ndio watahitimisha pale Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Shangwe ziliendelea kama kawaida katika tawi hilo, huku wakizipamba ofisi zao kuonyesha kuna tukio maalumu linataka kufanyika, pia walikuwa na ugeni kutoka Lindi na Songea waliokuja kuungana nao.

Mwenyekiti wa tawi hilo, Seifu Kobero anasema siku ya Simba Day kwao ina maana kubwa, akidai inawapa taswira ya namna ambavyo msimu utakavyokuwa kwa upande wao.

Chanzo: mwananchi.co.tz