Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba SC yatoa mchezaji bora wa VPL kwa mwezi Januari, 2018

Mon, 12 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Klabu ya Simba imetoa mchezaji bora wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara kwa mwezi Januari, 2018 ambapo mshambuliaji wake, John Bocco ametajwa kuwa ndiye mchezaji bora kwa mwezi huo.



 

Bocco amewashinda wachezaji wenzake akina Emmanuel Okwi na Awesu Awesu wa Mwadui kutokana na uchambuzi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za VPL.

Kwa mwezi Januari, Bocco ameisaidia Simba kupata pointi 9 katika michezo mitatu aliyocheza na kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi, huku akifunga mabao matatu na kutoa pasi mbili za usaidizi wa mabao.

Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa na Simba msimu huu amecheza dakika zote 270 za michezo mitatu ya Simba mwezi Januari huku akionesha kiwango kikubwa katika kila mchezo.

Chanzo: bongo5.com