Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba SC yaivutia kasi KMC FC

WhatsApp Image 2021 07 05 At 16.02.42.jpeg Simba SC yaivutia kasi KMC FC

Tue, 6 Jul 2021 Chanzo: dar24.com

Kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, leo Jumatatu (Julai 05) kimeanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba SC iliyopoteza mchezo wake dhidi ya Young Africans Jumamosi (Julai 02), itacheza na KMC FC keshokutwa Jumatano (Julai 07), Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.

Huenda mchezo huo ukawa mgumu sana kwa timu zote mbili, kufuatia hitaji la alama tatu muhimu kwa Simba SC ambayo inahitaji kutetea taji la Ligi Kuu, huku KMC FC wakihitaji alama hizo ili kuishusha Namungo FC kwenye nafasi ya tano.

Prince Dube hatarini kukosa Simba SCKMC FC ipo nafasi ya sita ikiwa na alama 42, ikitanguliwa na Namungo FC iliyo nafasi ya tano kwa kumiliki alama 42.

Simba SC inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na alama 73, na kama itashinda michezo yake miwili ijayo, itatangaza ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya nne mfululizo.

Manara kuacha kazi Simba SCSimba SC imesaliwa na michezo minne dhidi ya KMC FC, Coastal Union, Azam FC na Namungo FC.

Chanzo: dar24.com