Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba SC kuanzia nyumbani Ligi ya Mabingwa

33963 Pic+simba Kikosi cha Simba

Sat, 29 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

 Mabingwa wa soka Tanzania, Simba wamepangwa na miamba ya soka Misri, Algeria na Tunisia kuwania ubingwa wa Afrika mechi zitakazoanza baadaye Januari.

Hiyo ni baada ya droo iliyochezeshwa jana mjini Cairo, na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Kwa mujibu wa droo hiyo ambayo ilishuhudia na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Abdallah Salim ‘Try Again’ Simba imepangwa Kundi D. za kundi hilo ni Al Ahly ya Misri, JS Saoura ya Algeria na AS Vita ya DR Congo.

Ratiba hiyo inaonyesha kuwa mechi ya kwanza Simba itaanzia nyumbani kucheza na JS Saoura nyumbani baadaye Januari.

Mbali na ligi hiyo ya mabingwa, CAF imetangaza ratiba ya Kombe la Shirikisho ambalo Gor Mahia ya Kenya itaanza na New Star ya Cameroon wakati Al Ahly Benghaz ya Libya itakwaana na Hussein Dey ya Algeria.

Mechi nyingine itazikutanisha El Hilal ya Sudan itakayopambana na Mukura Victory ya Rwanda. Kundi la nne, Nkana FC ya Zambia waliotolewa na Simba wamepangwa kucheza na FC San Pedro ya Ivory Coast. Cotton Sport ya Comeroon itaonyesha kazi na Asante Kotoko ya Ghana huku Zesco FC ya Zambia itakwaruzana Kaizar Chiefs ya Afrika Kusini. Kundi lingine, Stade Malien ya Mali itacheza na Atletico ya Angola. Raja Casablanca ya Morocco itashuka Kusini mwa Afrika kuifuata African Stars ya Namibia. RS Berkane ya Morocco imepangwa na ASC JERAF ya Senegal. Kigogo kingine, CS Sfaxien ya Tunisia itaanza na Vipers ya Uganda kabla ya Zamalek kukumbana na IR Tanger ya Morocco. KCCA itacheza na VC As otoho d’oyo ya Congo wakati Bantu FC ya Lesetho itaikaribisha Rangers ya Nigeria. Al Nasri ya Libya itakuwa nyumbani kuikaribisha Saltas FC ya Burkina Faso kabla ya . Jimmara Aba ya Ethopia kucheza na Hasania us Agadir ya Morocco.

Kauli ya wadau

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mbarak Abduwakil alikataa kuzungumzia suala hilo, akidai kuwa amebanwa na vikao ofisini kwake.Hata hivyo, Kaimu Ofisa Uhusiano wa Uhamiaji, Tatu Burhan alikiri kuwepo kwa tatizo hilo, lakini akasema halitokani na mashine zao kuharibika.





Chanzo: mwananchi.co.tz