Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba SC haijawahi kuwaacha salama Marais Tanzania

98542 Magufuli+pic Simba SC haijawahi kuwaacha salama Marais Tanzania

Tue, 10 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kipigo cha bao 1-0 ilichokipata Simba kutoka kwa Yanga jana kwenye Uwanja wa Taifa, kimeendeleza nuksi ya mabingwa hao kila wapocheza mbele ya Marais wa Tanzania.

Hii ni mara ya tatu mfululizo Simba ikiwa na kikosi bora, lakini inapocheza mbele ya Marais wa Tanzania imekuwa ikiambulia kichapo cha aibu.

Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 1993 ambapo Simba walipoteza mchezo wa fainali ya Kombe la CAF nyumbani dhidi ya Stella Abidjan ya Ivory Coast kwa mabao 2-0.

Mchezo huo ambao ulichezwa katika Uwanja wa Uhuru ambapo zamani ndio ulikuwa unaitwa Uwanja wa Taifa, ulihudhuriwa na Rais wa awamu ya pili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaji Ali Hassan Mwinyi.

Ikumbukwe kwamba Simba ilitoka sare ya kutofungana ugenini dhidi ya Stella Abidjan na ilikuwa inahitaji ushindi wa aina yoyote nyumbani ili itwae ubingwa.

Kipigo kingine cha Simba mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilikuwa ni mnamo Mei 19, 2018 walipochapwa bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar katika mchezo uliohudhuriwa na Rais Magufuli ambao pia ulikuwa ni mahususi kwa ajili ya kuikabidhi Simba kombe la ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2017/2018.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Jana Jumapili Machi 8, 2020 ikicheza mbele Rais Magufuli aliyekuwa mmoja wa mashabiki waliotazama mchezo huo walifungwa bao 1-0, lakini jana mbali ya Rais wa Tanzania alikuwepo Rais wa CAF, Ahmed Ahmed uwanjani hapo.

Rais Magufuli alikuwa amevaa jezi yake ambayo nusu ilikuwa na rangi ya Yanga na upande mwingine rangi nyekundu huku akiwa amevaa kofia yenye rangi ya bendera ya Tanzania.

Mshambuliaji Bernard Morrison alikuwa shujaa wa Yanga kwa kufunga bao pekee kwa mpira wa adhabu katika dakika 44 ya kipindi cha kwanza uliokwenda moja kwa moja wavuni na kumuacha kipa wa Simba, Aishi Manula akiruka bila matumani.

Chanzo: mwananchi.co.tz