Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Mwanza yaunda kamati kuimaliza Mtibwa Sugar

12101 PIC+MWANZA TanzaniaWeb

Wed, 15 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

MWANZA. MAMBO ni moto unaambiwa,wanachama na mashabiki wa Simba mkoani hapa wameamua kuunda kamati ya ushindi ya watu 15 watakaohakikisha timu hiyo inaibuka na ushindi katika mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mchezo huo unaotarajia kuchezwa keshokutwa Jumamosi kwenye uwanja wa CCM Kirumba,umeonekana kuwapa presha mashabiki wa Yanga na Simba jijini hapa.

Juzi viongozi wa matawi ya Yanga Mwanza walitangaza kuwaunga mkono Mtibwa Sugar ili kumuangamiza Mnyama,jambo ambalo limewashtua Simba na kuamua kuteua kamati ya ushindi ya watu 15.

Mwenyekiti wa kamati hiyo,Salya Ludanha alisema kuwa ili kuhakikisha wanashinda mchezo huo,wameamua kuunda kamati ya watu 15 kutoka matawi matatu.

Alisema kuwa katika kikao chao cha matawi yote 25 ya Mkoa wa Mwanza kilichoketi juzi waliazimia kuweka mkakati wa ushindi ili kuwazima wapinzani wao Yanga walioamua kuisapoti Mtibwa.

“Tulikuwa na kikao kizito juzi kilichohusisha matawi yote 25 ya mashabiki na wanachama wa Simba,ambapo tuliweza kuunda kamati ya ushindi ya watu 15 ambao watasimamia timu kupata ushindi”alisema Ludanha.

Kiongozi huyo aliongeza kuwa matawi waliyoteua kufanikisha zoezi hilo la ushindi ni Isamilo,Kawekamo na Nyegezi na kwamba mengine yapo kwa ajili ya kuongeza nguvu.

“Matawi yote tunashirikiana lakini tumeteua matatu ya Isamilo,Kawekamo na Nyegezi ambapo kila tawi tumetoa watu watano hawa wengine tuanendelea kushirikiana nao”alisema Kiongozi huyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz