Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Mwadui zaingiza Sh24milioni

19064 Kwatu TanzaniaWeb

Mon, 24 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Shinyanga. Mwadui imevuna Sh 24milioni pamoja na kupokea kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Simba katika mchezo uliochezwa jana Jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kambarage.

Katika mgawanyo wa fedha hizo Mwadui FC wenyeji wa mechi hiyo walipata Sh11 milioni, Simba wageni katika mechi hiyo wao hawakuambulia chochote kutokana na mabadiliko ya kanuni za ligi kwamba mapato yote atapata mwenyeji na sehemu zingine zinazotakiwa kama Bodi ya Ligi, FA.

Kiasi hicho kilitokana na idadi ya mashabiki 4876 watu wazima waliolipa kiingilio cha Sh 5000 wakati watoto walioingia 222 wakilipa Sh 2500.

Idadi hiyo ya mashabiki ilikuwa ndogo ukilinganisha na msimu uliopita, hii inadaiwa kuchangiwa na matokeo mabaya ya Simba waliyoyapata katika mechi zao mbili zilizopita kabla ya kucheza na Mwadui ambapo walishinda bao 3-1.

Chanzo: mwananchi.co.tz