Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba: Msihofu Wametushikia Nafasi Yetu

Simba Shukrani Simba: Msihofu Wametushikia Nafasi Yetu

Thu, 17 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya Yanga kuongoza Ligi Kuu Bara kwa tofauti ya alama tano, aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba, Hassan Dalali, amesema kuwa Yanga imewashikia kwa muda tu nafasi yao.

Yanga kwa sasa wako kileleni mwa ligi kuu wakiwa na pointi 36 baada ya kushuka dimbani mara 14 ambapo wameshinda mechi 11 na sare tatu.

Simba wao wamecheza mechi 15, wameshinda tisa, sare nne na kupoteza mbili wako nafasi ya pili na alama zao 31.

Dalali alisema kuwa: “Kuhusu ubingwa wa Ligi Kuu Bara hilo halina ubishi wale wenzetu wametushikia nafasi yetu na muda utakapowadia tunakwenda kuwashusha na safari ya ubingwa itaanzia hapo, kikubwa tuwe wamoja tusitengeneze makundi ambayo yatakuja kutuvuruga na tukatoka kwenye malengo yetu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live