Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Mbao FC mechi ya malengo

Mbao FcKL 1 Mbao FC

Thu, 16 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

TUNATAKA heshima! Hayo ni maneno ya Kocha Mkuu wa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, Sven Vandenbroeck kuelekea mchezo wa ligi hiyo dhidi ya Mbao FC kutoka Mwanza utakaochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini, Dar es Salaam.

Sven aliliambia gazeti hili jana anahitaji kupata pointi tatu katika mchezo huo ili kuendelea kuupa heshima ubingwa wa msimu huu wa 2019/20, ambao wameshautwaa.

Kocha huyo alisema baada ya mapumziko ya siku mbili, kikosi kilirejea kwenye mazoezi jana asubuhi na anaamini nyota wake watakuwa na nguvu mpya ya kusaka ushindi katika mchezo huo dhidi ya Mbao ambayo inahitaji pia pointi ili kujiondoa kwenye hatari ya kushuka daraja.

"Tunahitaji kumaliza ligi tukiwa na pointi nyingi, hivyo tunaenda kufanya kazi kuhakikisha wachezaji wanatafuta matokeo, tunajua Mbao FC wako katika hali mbaya, lazima wataingia na nguvu," alisema Sven.

Naye nahodha wa Simba, John Bocco, alisema: "Mbao ni timu nzuri ingawa wako katika nafasi mbaya, hivyo watakuja kutafuta matokeo, lakini kwa upande wetu tunahitaji kukusanya pointi katika michezo yote iliyobakia," alisema Bocco.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live