Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, KMKM zakumbushia Ligi ya Muungano

35091 Pic+simba Simba

Mon, 7 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Simba imecheza juzi Ijumaa na kuilaza Chipukizi 4-1, leo Jumapili wana kibarua kigumu dhidi ya wanajeshi wa Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo (KMKM), mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Amaan usiku wa saa 2.15 Kocha wa Simba Patrick Aussems alisema ratiba inawabana kwani mechi zimeongozana lakini kutokana na upana wa kikosi chake hana hofu kuwavaa wanajeshi hao.

Wakati Aussems akitambia kikosi chake kocha wa KMKM, Ame Msimu naye amegawa kikosi chake kilichocheza jana Jumamosi na kitakachowavaa Simba leo. Simba na KMKM zimekutana mara kadhaa enzi ya Ligi ya Muungano.

Msimu alisema anafahamu anakutaka na timu kubwa na ngumu lakini mpira ni dakika 90 zenye kuamua kwani hata kama watapoteza mechi si kirahisi kama ambavyo mashabiki wanachukulia.

“Hakuna anayependa matokeo mabaya kila mmoja anajipanga kwa ushindi hata hao Simba ni hivyo hivyo, tunaingia kucheza na Simba tukiwa hatujapumzika ila sio tatizo kwetu.

“Sisi ni wanajeshi ambao tumezoea hata kucheza mechi mbili kwa siku ili mradi tuwe na kikosi kipana, KMKM ina wachezaji wengi kuna wale ambao wanacheza mechi ya leo (jana) na wengine wanacheza leo (Jumamosi) na Simba ingawa wengine waliocheza jana wataongezwa” alisema

Yoyote Simba ni mwanajeshi

Nyota kibao wa Simba juzi Ijumaa hawakucheza dhidi ya Chipukizi walipopata ushindi wa mabao 4-1

Aussems anasema, “Mechi za mashindano haya zipo karibu karibu hivyo ni lazima uwe makini katika matumizi ya wachezaji, niliwaacha wengine ambao ninaamini watacheza mechi hii ya KMKM.

“Tunaheshimu kila timu kwenye haya mashindano hata wachezaji wangu nawaeleza juu ya hilo, kikubwa lakini kwetu ni kama nilivyosema awali tunaangalia zaidi michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema Aussems Simba ndiyo inaongoza Kundi A kwenye michuano hiyo ikiwa na pointi tatu na magoli manne huku mchezaji wao Nicolas Gyan akiongoza kwa mabao akifunga mawili.



Chanzo: mwananchi.co.tz