Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Hakuna Sauti Ya Mamlaka, Hii Itawakosti

Simba ,kocha Mpya Simba vs Coastal

Mon, 1 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa misimu kadhaa iliyopi nilipoitazama Simba hata kama ilipoteza mchezo au sare, bado kulikuwa na muunganiko wa timu kucheza kwa kujua wanataka nini.

Kwa lugha ya kimichezo walikuwa na chemistry nzuri ndani hadi nje ya uwanja, uwepo wa Mohamed Dewji ‘Mo’ ambaye aliwekeza fedha uliifanya klabu hiyo kuwa tishio.

Fedha za Mo na wenzake ziliituliza #Simba kotekote, benchi la ufundi, wachezaji na katika uongozi.

Nguvu hiyo ikawafanya wasajili wachezaji wenye uwezo wa juu wakilipwa vizuri, ndiyo maana naweza kukubaliana na alichokisema wakati ule, kiungo mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison kuwa Simba ni Chuo Kikuu cha Soka Tanzania.

#Morrison alisema hivyo kwa kuwa uwepo wa mtu kama Clatous Chama kikosini kuliwafanya wapinzani waone #Simba wana mtu hatari, hata ilipotokea timu inazidiwa Chama hakuonyesha kuwa na papara na akawafanya wenzake kufuata mamlaka ya kile alichokuwa miguuni mwake.

Siyo kwamba Simba ilikuwa haifungwi kila Chama alipocheza, lakini uwepo wake uliwafanya wachezaji wengine wawe na mamlaka wakiamini wao ni wakubwa na wanastahili kucheza soka la kikubwa.

Simba ya sasa, haina Chama, utulivu katika benchi la ufundi umepotea, viongozi nao hakuna mwenye nguvu ya mamlaka kama ilivyokuwa kwa Mo ambaye nguvu ya fedha zake tu iliwafanya wachezaji na mashabiki kutembea kifua mbele hata pale walipokutana na timu kubwa zaidi yao.

Simba ya sasa haina mabadiliko makubwa kikosini lakini hakuna mtu au watu wenye mamlaka ya kusema wanaibeba timu mgongoni, kuanzia kwa wachezaji hadi kwa uongozi.

Kufungwa au sare ni kitu cha kawaida, lakini tazama mchezo dhidi ya Coastal Union, benchi la ufundi la Simba vikao vingi, kila mtu anatoa ushauri, sura za viongozi wao jukwaani ‘body language’ inaonyesha kama hawana matumaini.

Ndani ya uwanja wachezaji wanapambana lakini hakuna mmoja wa kusema ‘leteni mpira hapa’ niitulize timu.

#Bwalya ni mzuri na amekuwa na msaada mkubwa lakini bado hajafanikiwa kuwa na mamlaka ya kuiweka timu begani.

Simba inahitaji mamlaka kotekote kwa wachezaji, benchi la ufundi na kwa uongozi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live