Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba: Eeh Mungu tusaidie

Mungu Pic Data Simba: Eeh Mungu tusaidie

Sat, 22 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KWA namna yoyote ile kwa Mkapa hatoki mtu. Historia ya Simba kimataifa inathibisha. Na leo kocha Didier Gomes amepanga fomesheni moja balaa, wale jamaa mbona hawatoki!

Wekundu wa Msimbazi hawana namna wala lugha yoyote inayoweza kuwavusha zaidi ya leo kuwapiga nyingi Amakhosi ili kusonga mbele. Na Wanamsimbazi wote wanajua kwamba wasipowapiga nyingi Kaizer safari yao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu itaishia leo kutokana na kuruhusu mabao 4-0 ugenini.

Sasa kocha Gomes kalisuka chama lake katika fomesheni mbili za kufa mtu na lazima kieleweke. Yaani ni Ama Zetu Ama Zao, hii ni Do or Die Season Two.

Yaani plani ya kwanza ni kumpiga nyingi Kaizer na kufuzu nusu fainali, lakini jambo hilo likishindikana mpango ni kuwapasua wapinzani wao hao ili kuweka heshima maana hawako tayari kudhalilika kwenye uwanja wa nyumbani.

Simba ina rekodi ya kibabe sana kwenye uwanja wa nyumbani. Haijapoteza mchezo tangu Februari 17, 2013 walipofungwa 1-0 na Reacreativo do Libolo ya Angola kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kufikia leo ni miaka 8, miezi mitatu na siku tano (sawa na siku 3,016) zimepita bila ya Simba kupoteza mechi ya kimataifa kwenye Uwanja wa Mkapa. Hawa Kaizer wanatokaje sasa?

Katika kukamilisha hicho ambacho wengi wanakiona kama ni ‘Mission Impossible’, kocha Didier Gomes, huenda akabadilisha mfumo wake pendwa wa 4-2-3-1 na kwenda kucheza mingine miwili tofauti 4-4-2 na 4-3-3.

Kwa mujibu wa mazoezi ya mwisho, mfumo wa kwanza wa 4-4-2, Gomes huenda akaanza na mabeki wanne, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Joash Onyango, Pascal Wawa.

Kwenye eneo la kiungo atakuwa na Taddeo Lwanga, Clatous Chama, Luis Miquissone na Bernard Morrison ambaye hakuwepo kabisa katika mechi ya kwanza na ana usongo kinoma wa kutupia leo.

Morrison anapewa nafasi ya kuanza kutokana na ubora alionyesha mazoezini lakini pia uwezo wake mkubwa katika kushambulia anapokuwa na mpira, kuwasumbua mabeki na kufunga mabao ya aina mbalimbali.

Simba wanahitaji kushambulia zaidi ndio maana Morrison huenda akapewa nafasi ya kuanza sambamba na mastraika wawili nahodha John Bocco na Chriss Mugalu.

Mfumo mwingine wa 4-3-3, ambao Simba unakuwa na mabeki wanne wataanza wale wale ila katika kiungo watakuwepo Lwanga, Chama na Mzamiru Yassin ambaye hakucheza mechi ya kwanza. Jonas Mkude hayupo kabisa kambini na atakuwa jukwaani.

Watatu wa mbele watakuwa Mugalu, Bocco na Miquissone, ambaye ndiye mfungaji bora wa kikosi hicho katika hatua ya makundi akifunga mabao matatu.

Kutokana na mabadiliko hayo ya kimfumo maana yake wachezaji ambao walianza mechi iliyopita ila huenda isiwe hivyo leo ni, Mkude na Larry Bwalya ambaye atakuwa benchi akiusoma mchezo na kusikiliza shangwe za mashabiki 10,000.

Kulingana na mazoezi ya Simba, kikosi ambacho kinaweza kuanza katika mechi ya leo saa 10 jioni kitakuwa hivi, Aishi Manula, Kapombe, Tshabalala, Onyango, Wawa, Lwanga, Morrison/Mzamiru, Chama, Mugalu, Bocco na Miquissone.

Kwa upande wa Gomes, alisema wanaingia katika mechi hiyo wakiwa wamebadilisha mbinu zote. “Tunahitaji kubadilika na kuwa bora ndio maana hata mbinu na aina ya uchezaji itakuwa tofauti katika mechi hii ili kupata kile ambacho tunahitaji kwani katika soka kila kitu kinawezekana,” alisema Gomes.

Kiraka wa Simba, Erasto Nyoni alisema “Kama wachezaji mechi tunaitaka kweli na tumedhamiria kupindua matokeo.”

Mzee wa kuwakera, Morrison alisema “Nipo vizuri na tayari kwa ajili ya mchezo.”

KWA MAONI TUTUMIE KWENYE NAMBA 0658-376 417

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz