Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Day uwanja wa Taifa watapika mapema tu

70210 Simba+ua+picha

Wed, 7 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Simba imeamua kujibu mapigo ya watani wao wa jadi Yanga, ambao Jumapili walijaza Uwanja wa Taifa, kuhitimisha wiki ya Mwananchi, kwani wingi ya mashabiki wa Msimbazi ipo taifa kuhitimisha 'Simba Day'.

Simba Day ilianzishwa mwaka 2009 chini ya aliyekuwa mwenyekiti wa timu hiyo, Hassan Dalali lengo likiwa ni kukusanya fedha za kujenga uwanja, kukutanisha mashabiki toka mikoa ya Tanzania, kuwatambulisha wachezaji na kufanya shughuli za kijamii.

Imekuwa tofauti na matarajio ya wengi kudhani mashabiki wa Simba wangekuwa kiduchu kutokana na tamasha hilo limeangukua siku ya kazi, wamejitokeza kwa wingi ambao nje ya uwanja kuna msululu wa watu unafuata foleni ya kuingia ndani.

Huu ni mwaka wa 10 kwa Simba kufanya tamasha hilo, ambapo mashabiki watapata muda wa kufahamiana na wachezaji ambao watafanya nao kazi msimu ujao wa 2019/20.

Ukiachana na msululu wa watu ambao unasubiri kuingia ndani, tayari kuna watu ambao walifika mapema na kuziwahi siti za kukaa na kusubiria tamasha lenyewe kuanza.

Askari nao hawapo nyuma kufanya kazi yao kuhakikisha mashabiki wanakuwa salama, wanaelekeza wale wanaoingia na kusimamia foreni ili aliyewahi aweze kupata haki zao.

Asilimia kubwa ya mashabiki wamevaa jeziĀ  nyekundu huku ile yenye mchanganyiko ikivaliwa na wachache Wao.

Licha ya wachache wao kuvaa jezi mpya, kundi kubwa limeonekana kuwa na jezi ambazo zilitumika msimu uliopita wakati Simba ikibeba ubingwa wa Ligi Kuu.

Chanzo: mwananchi.co.tz