Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Azam zaziba njia Majimaji

Kuziba Njia Pic Data Simba, Azam zaziba njia Majimaji

Sat, 26 Jun 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kuelekea kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la Azam (ASFC), kati ya Azam na Simba uliopangwa kupigwa saa 9:30 jioni, kwenye uwanja wa Maji maji Songea, tayari mashabiki wamejazana kwenye barabara zinazozunguka uwanjs huo.

Ikiwa ni Saa tatu za asubuhi, licha ya hali ya hewa ya Songea kuwa na baridi kali lakini mashabiki wengi wa Simba, Azam na wadau wengine wa soka wamepanga misitari kwenye barabara za nje ya uwanja wakisubiri milango ifunguliwe waweze kuingia ndani.

Kujaa huko kwa mashabiki katika bara baea hizo kumesimamisha shughuli za usafirishaji kupitia barabara hizo kwani hakuna gari inayopita kutokana na watu kuwa wengi katika barabara hizo.

Sambamba na hilo pia viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Simba, Azam na wanahabari wameonekana kwa wingi mjini Songea kila mmoja akitekeleza majukumu yake.

Mshindi wa mechi ya leo atakutana na Yanga kwenye mchezo wa fainali baada ya wanajangwani hao kutinga fainali jana kwa kuifunga Biashara United bao 1-0, kwenye mechi ya nusu fainali iliyochezwa mkoani Tabora.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz