Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Azam zaondolewa kupiga kura uchaguzi TFF

TFF Logo 1 Simba, Azam zaondolewa kupiga kura uchaguzi TFF

Sat, 7 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Klabu za Simba na Azam zimekosa uwakilishi na kuondolewa kwenye mchakato wa kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) unaofanyika leo Jumamosi Agosti 7, 2021 jijini Tanaga.

Wakati wa kuhakiki majina ya wapigakura, alitajwa rais wa Simba, Murtaza Mangungu kama yupo, na mkutano ukageuka kuangaza na hakuna aliyesema kama yupo huku baadhi ya minong'ono ikitawala.

Alipotajwa mpiga kura wa klabu ya Azam, Nasoro Idrisa pia hakuwepo na mwenyekiti kutaka wakatwe kwenye orodha ya wapiga kura.

"Hatutaki kura za maruhani hapa," alisema Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi ya shirikisho hilo, Wakili Kiomoni Kibamba

Hata hivyo baadhi ya wajumbe walidai Nasoro ametuma mwakilishi.

Mpiga kura mwingine aliyekatwa ni kutoka Chama cha soka Shinyanga Ibrahim Kani huku Said Makirigo akiwa mpiga kura pekee wa FA ya Shinyanga.

Wakati wowote kuanzia sasa kura zitaanza kupigwa, ikianza na ile ya rais ambaye atahidhinishwa na mkutano mkuu kabla ya wagombea 17 wa ujumbe kupigiwa kura.

Imeandikwa na Raisa Said na Imani Makongoro

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz