Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Azam wajaza uwanja mapema

Simbasctanzania 189560407 2872443659674816 422397598469859582 N?fit=800%2C533&ssl=1 Simba, Azam wajaza uwanja mapema

Sat, 26 Jun 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MUDA mchache kabla ya mechi ya nusu fainali ya kombe la Azam (ASFC), kati ya Azam na Simba kuanza kwenye uwanja wa Majimaji, Songea tayari mashabiki wamejaa katika majukwaa yote wakisubiri kuanza kwa mtanange huo.

Mwanaspoti imethibitisha hilo saa 7:40 uwanja huo ulikuwa tayari umefurika mashabiki wa timu hizo mbili huku wale wa Simba wakionekana kuwa wengi kuliko wenyeji Azam.

Dakika sita baadae basi msafara wa Azam ukiongozwa na gari la Askari uliingia uwanjani hapo na kuamsha shangwe kutoka kwa mashabiki.

Mbwembwe ziliendelea uwanjani hapo na mashabiki wengine wakiendelea kuingia huku nje foleni ya mashabiki ikionekana kuendelea kuwa kubwa zaidi.

Mtanange huo unayarajiwa kuanza saa 9:30 jiono na mshindi atatinga fainali kukutana na Yanga iliyofuzu jana baada ya kuichapa Biashara United bao 1-0 kwenye mchezo wa nusu fainali uliofanyika mkoani Tabora.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz