Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shule maalum ya vipaji vya michezo kujengwa Ilala

Shule Ilala Shule maalum ya vipaji vya michezo kujengwa Ilala

Mon, 19 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Serikali inatarajia kujenga shule ya sekondari maalumu yenye vipaji vya michezo eneo la Mvuti wilaya ya Ilala ambayo itasaidia kuinua michezo mbalimbali nchini.

Mkuu wa wilaya ya Ilala, Mwilabuzu Ludigija akizungumza hayo wakati akizindua bwalo la gereza Kambi Mvuti, alisema itaanzishwa shule maalumu ya vipaji vya michezo na itajenga viwanja mbalimbali vya michezo ili watoto waweze kubitumia.

Ludigija alisema lengo la kujenga shule hiyo kuwafundisha watoto ili kupata vipaji maalumu itakayosaidia kuinua michezo nchini ili washiriki kwenye makombe mbalimbali ikiwemo mpira wa mguu.

"Hii shule itafundisha michezo mbalimbali itajengwa viwanja mbalimbali vya kisasa ambavyo vitatumika kuwafundisha watoto watakaosoma katika shule hiyo na huo ni mpango wa serikali kuwa na shule maalumu za kufundisha vipaji vya michezo,"alisema Ludigija.

Afisa elimu Sekondari jiji la Ilala,Musa Ali alisema wana hekari 40 ambapo wanatarajia kuanzisha shule ya sekondari kidato cha tano na sita pamoja na shule maalumu itakayochukuwa watoto wenye vipaji vya michezo.

Alisema fedha kiasi cha Sh 50 milioni imetengwa na halmashauri ya jiji hilo kwa ajili ya kujenga shule maalumu pamoja na viwanja vya michezo.

"Hapa tunasubilia fedha kiasi cha Sh50 milioni kutoka halmashauri tukizipata tu tutajenga viwanja vya mpira vya shule maalumu ya sekondari Mvuti ambapo hadi sasa hivi tumejenga mabweni matatu na madarasa 12," alisema Ally

Naye Mkuu wa gereza hilo Jastine Kipeta amesema wamezindua bwalo la gereza Kambi Mvuti ambalo limegharimu kiasi cha Sh50 milioni litatumika kwa shughuli mbalimbali ikiwemo burudani na sherehe.

Chanzo: Mwanaspoti