Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shughuli kamili ya watani hii hapa

42144 Pic+kamili Shughuli kamili ya watani hii hapa

Mon, 18 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KUNA kila sababu kwa mashabiki wa soka jijini Dar es Salaam kujongea hadi pale Uwanja wa Taifa kutazama pambano la watani wa jadi, Yanga na Simba litakalochezwa kwenye Uwanja wa Taifa leo Jumamosi.

Kwa wale wa nje ya Dar es Salaam na wengine ambao hawatapata fursa ya kwenda Uwanja wa Taifa leo, wanapaswa kujisogeza jirani na runinga zao ili wafaidi uhondo na mshikemshike wa mechi baina ya timu hizo mbili kongwe nchini.

Ngassa vs  Coulibaly,

Mrisho Ngassa ana uzoefu mkubwa wa kucheza mechi za watani wa jadi akiwa ameifungia Yanga, mabao matatu kwenye mechi zinazoutanisha timu hizo na kuelekea kwenye mchezo wa leo, uzoefu na ubora wake utakuwa majaribuni mbele ya beki, Zana Coulibaly kutoka Ivory Coast ambaye licha ya kutoanza vizuri ndani ya Simba siku za hivi karibuni ameonyesha kuimarika na alifanya vyema kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ambao timu yake ilishinda kwa bao 1-0.

Tambwe vs Juuko

Amissi Tambwe amefunga mabao matatu kwenye mechi baina ya timu mbili hizo kongwe hapa nchini. Akiwa Simba aliifunga Yanga bao moja na alipohamia upande wa pili akafunga mabao mawili dhidi ya waajiri wake wa zamani. Leo anakutana na kibarua kizito mbele ya beki mbabe na mzoefu wa Simba, Juuko Murushid ambaye anasifika kwa uwezo wake wa kukabiliana na washambuliaji wa timu pinzani.

Makambo vs Wawa

Makambo hadi sasa amepachika mabao 11 kwenye Ligi Kuu na kuongoza chati ya ufungaji bora lakini ubora wake anapaswa kuuthibitisha mbele ya beki wa miraba minne, Wawa ambaye amekuwa kiongozi wa Simba kwenye safu ya ulinzi.

Tshishimbi vs Kotei

Papy Tshishimbi ameonekana kupungua ubora tofauti na alipojiunga nayo. Hata hivyo, atalazimika kufanya kazi ya ziada leo mbele ya kiungo mkabaji mwenye mapafu ya mbwa wa Simba, James Kotei wakati watakapokabiliana.

Ajibu vs Tshabalala

Mpishi wa mabao ya Yanga msimu huu ni kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajibu. Ili Simba iibuke na ushindi leo kwa kiasi kikubwa inatakiwa kuhakikisha inamficha Ajibu ambaye hadi sasa amefungwa mabao sita na kutoa pasi za mwisho 13.

Jukumu hilo kwa Simba leo limeangukia kwa beki na Nahodha Msaidizi, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ ambaye alishawahi kucheza naye pamoja kabla Ajibu hajatimkia Yanga.

Fei Toto vs Mkude

Ni vita ya mafundi wawili wa kuuchezea mpira ndani ya uwanja, uwezo wa kupiga mashuti na pasi ambazo zimekuwa zikiwafikia walengwa kwa usahihi.

Feisal Salum ‘Fei Toto’ ni mtaalamu wa kupiga pasi ndefu wakati Mkude ni mtaalamu wa kupiga pasi fupi, hivyo ni wazi yule atakayefanikiwa kumfunika mwenzake pale katikati mwa kiwanja, atakuwa na nafasi kubwa ya kuifanya iibuke na ushindi.

Yondani vs Bocco

Nyota wawili wenye uzoefu wa mechi kubwa watakuwa na shughuli pevu ya kuzisaidia timu zao pindi zitakapokutana leo.

Huu utakuwa ni msimu wa pili kwa Bocco kucheza echi za watani wa jadi lakini tayari alishakutana na kuifunga Yanga mara nyingi pindi alipokuwa Azam FC lakini pia Yondani amecheza mechi hizo tangu mwaka 2008.

Ninja vs Kagere

Baada ya kunusurika kutocheza mechi ya leo, beki Abdallah Shaibu ‘Ninja’ leo atakuwa na kazi nzito ya kumdhibiti mshambuliaji tishio nchini kwa sasa, Meddie Kagere. Kagere ameshaifungia Simba mabao saba kwenye Ligi Kuu na pia amepachika mabao sita kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Gadiel vs Okwi

Hapana shaka na ni jambo lililo wazi kuwa straika Emmanuel Okwi anazijulia mechi hizi ambazo zimekuwa awe kipenzi cha mashabiki wa Simba. Usalama kwa Yanga utakuwepo kwa asilimia kubwa iwapo watamfanya Okwi asipate nafasi ya kuonyesha makeke yake jukumu ambalo litaangukia kwa beki, Gadiel Michael.inazokutanisha Simba na Yanga, Okwi amepachika mabao manne.

Boxer vs Chama

Beki chipukizi, Paul Godfrey ‘Boxer’ aling’ara kwenye mechi ya kwanza baina ya timu hizo ambap;o iliisha kwa timu hizo kutoka sare tasa, lakini leo atatakiwa kudhihirisha ubora wake mbele ya kiungo mshambuliaji mjanja, Clatous Chama.

Chama ndiye amekuwa mhimili wa safu ya ushambuliaji ya Simba kutokana na uwezo wake wa kuchezesha timu, kupiga pasi za mwisho, kubomoa ukuta wa timu pinzani na kufunga mabao.



Chanzo: mwananchi.co.tz