Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shonza ataka viongozi wa mpira kuacha maslahi binafsi

68434 Pic+shonza

Sun, 28 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mtwara. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania, Juliana Shonza amewataka viongozi wanaosimamia suala nzima la mpira wa miguu kubadilika na kuachana na maslahi binafsi ili kuondokana na migogoro lakini pia kupata matokeo chanya.

Shonza ameyasema hayo leo,Julai 26,2019 mkoani Mtwara na kusisitiza mahali popote ambao mtu anatanguliza maslahi binafsi mbele bada ya kuweka uzalendo mbele mafanikio yanakuwa hayapo na badala yake kurudi nyuma.

“Tusipofanya hivyo kila siku itaendelea kuwa ni migogoro, kuendelea kulumbana na kutupiana lawama ambazo zitakuwa hazina msingi lakini mataifa mengine yataendelea kupiga hatua mbele sisi tutabaki ni watu wa kulaumu, unamlaumu huyu huyu naye anamtupia mpira huyu,” amesema Shonza

Amesema kwa kufanya hivyo yatakuwepo mabadiliko na kushuhudia maendeleo makubwa kwenye soka na kwamba Serikali inayo mipango mizuri kuhakikishia inasimamia mpira wa miguu nchini kwa kutekeleza sera ya michezo ya mwaka 1995 ambayo wizara iko katika hatua za awali kuweka na kutengeneza mpango mkakati utakaoshirikisha serikali na wadau mbalimbali.

 

“Kuna kipindi kelele zilianza sera ya michezo imepitwa na wakati sisi kama serikali tukalifanya kazi lakini likaonekana ile sera imekidhi vigezo na ina sifa zote za kuweza kusimamia michezo nchi, kitu ambacho kilikuwa kinakosekana ni mpango mkakati kuweza kuitekeleza sera na utakapokamilika naamini utaleta matokeo mazuri katika soka letu,” alisema

Pia Soma

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz